Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

sasa hii gesi inasemekana kuna bacteria wasioonekana kwa macho ambao hawatumii Oxygen hua wanaishi katika gesi hii na kwa sababu gesi hii ipo katika sayari ya Venus huenda sasa bacteria hawa wapo wanaishi ndani ya gesi hii au huenda wenyewe ndio wanaitengeneza..
 
ni ngumu kuthibitisha kua viumbe hawa wapo au kufanya chunguzi zingine katika sayari hii maana ni ngumu sana hata kuona yaliomo ndani ya sayari hii sababu imejaa hewa nzito yenye Carbon dioxide ya kutosha pamoja na mawingu mazito yenye gesi nzito kama sulfuric acid na zinginezo.
 
Ukiwa hapa duniani unaweza kupiga kelele yoyote ile na kila mtu akakusikia mfano 🗣Mkaa! 🗣Mkaa!.... Lakini je wajua kua ukiwa angani nje ya hii dunia yetu, hata upige kelele vipi sauti yako haiwezi kufika popote pale hata rafiki yako ambae anaweza kua pembeni yako hata kusikia.
 
Sasa angani huko katika uwazi mkubwa, katika nafasi tupu isio na sayari wala nyota yeyote ile.. katika sehemu hii hata ukiongea kwa sauti gani mtu yoyote yule hawezi kukusikia sababu sehemu hii haina kitu chochote yani ni tupu na hamna chembe chembe za hewa kwahiyo sauti yako haiwezi kusafiri maana chembe chembe za hewa(Air molecules) ndio kama barabara ya sauti kupita lakini hapo katika Anga tupu chembe chembe hizo hazipo.
 
Mwanaanga mmoja akiongea hicho kifaa katika Helmet yake kinabadilisha sauti kuwa katika mawimbi ya redio na kuyasafirisha mpaka kwa mwanaanga mwenzake ambae nae anakifaa ndani ya Helmet yake kwa ajiri ya kuyapokea mawimbi hayo na kuyabadilisha kuwa sauti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…