Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

TUMIA AKILI YA KAWAIDA TU

Hivi kwanini CAG hajaigusa Ofisi ya makamu wa Rais , kipindi hicho Mama alikuwa huko, tuseme yenyewe haikuwa na matumizi?.......

Fikria Tena kwanini hawajaigusa ofisi ya WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, kipindi hicho alikuwa Kaka yetu ambae saizi Ni Makamu, tusema Ofisi yake haikuwa na matumizi ?.......


TUTAVURUGWA VURUGWA HADI LINI?
 
Kuna KASIMA nyingi tu zimekwepwa. Taaluma yetu imegeuzwa kuwa njia ya kupitishia matakwa ya wanasiasa.
 
Kuna KASIMA nyingi tu zimekwepwa. Taaluma yetu imegeuzwa kuwa njia ya kupitishia matakwa ya wanasiasa.
Mimi kinachonisikitisha ni kwamba (hata kama yote yaliyotajwa na CAG ni ya kweli), tunachomokaje katika utamaduni huu wa kuiba mali ya umma namna hii? Enough is enough jamani! Japo mjadala umejikita kwenye kumponda mwendazake (kitu ambacho hakitusaidii sana japo nadhani pengine ndiyo lengo kuu), hakuna popote tunapojaribu kuja na masuluhisho ya maana. Miaka nenda miaka rudi ufisadi uko pale pale tu. Kwa hali iliyopo sasa, hata aje nani kutuongoza ulaji utaendelea tu kwa sababu inavyoonekana wakwapuaji hawa hawaogopi. Hawaogopi kutumbuliwa. Hawaogopi vifungo. Yaani hawaogopi! Na hata tukipata rais mwadilifu kabisa kabisa (kama alivyokuwa Nyerere) upigaji utaendelea tu kwa sababu rais hawezi kuwa mahali pote kama watendaji wake ni wabovu - na jamii inawategemea kuwa wabovu. Wezi!

Madudu hayo yameanikwa. Unafikiri waliotajwa watafanywa nini? Hakuna kitu. Zitakuja siasa ndeefuu mpaka umma unasahau na miaka nenda miaka rudi tuko pale pale tu.

Going forward, tufanye nini ili angalau tujaribu kupunguza wizi huu wa mali ya umma? Ingefurahisha sana kama mjadala ungejikita kwenye kujibu swali hili muhimu. Tunaweza kweli tukafanikiwa kufuta legacy ya mwenda zake na tukafurahi sana na kupiga vigelegele, then what? Mwaka ujao, na ujao tena na ujao mambo ni yale yale na hata zaidi.

Kama jamii, we have to think out of the box. Rwanda kule nasikia ukifisadika mali zako zote zinataifishwa. Unafungwa. Na kama wazazi wako na ukoo wenu wote mnaambiwa kabisa kuwa litoto lenu ni lifisadi. Na kama kuna mali mlifaidika na litoto lenu hilo fisadi zinataifishwa pia. Kufisadika ni kuleta aibu kwa ukoo mzima. Na jamii imeanza kubadili fikra na kuanza kuchukia ufisadi. Hivyo mtu akitaka kuiba inabidi afikiri mara mbilimbili. Na matokeo yake ufisadi umepungua sana.

Huku kwetu bado ufisadi ni sifa. Iba sana. Jenga majumba hata 100. Hutafanywa cho chote. Badala yake utasifiwa na kuitwa mjanja mtoto wa mjini. Ukiwa mwadilifu kabisa kabisa ukaja kuyaachia madaraka hujatajirika hata jamii yenyewe haitakuelewa. Utachekwa kama ambavyo Mzee Mangula huwa anachekwa. Au Nyerere na watoto wake wanaoishi maisha ya kawaida tu. Utawezaje kuutokomeza ufisadi katika mazingira haya na jamii ya aina hii?

Acha leo tushangilie sana. Na mwaka kesho ni yale yale (na hata zaidi)...na maisha yanaendelea....


 
Ngoja niipeleke sehemu hii
 
Raha yao ni kumnanga mwendazake pekee hayo mengine wala hawajali kabisa. Na wapo busy kuhakikisha kila mradi wa magu unadondoka ili rohi zao zifurahi kuwa hajaacha alama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…