Mafigo hufanya kazi muhimu kwenye miili yetu kama kuondoa sumu, kuchuja damu na kufyonza madini. Uharibifu wa figo unaweza usigundulike kwa miaka mingi kwa maana figo huweza kufanya kazi hata kwa 20% ya uwezo wake
UTAFITI: Kuamini mpenzi/mwenzi wako anakupenda kuna faida kwa afya yako na kuongeza siku za kuishi. Watafiti wamedai uwezo wa kukabiliana na mkazo (stress) hupungua pale unapokuwa kwenye mahusiano na mtu usiyemwamini
Angalau dakika 60 za mazoezi, masaaa 9 hadi 11 ya usingizi wa usiku na kuangalia televisheni chini ya masaaa 2, mapendekezo haya matatu yanahusishwa na ufaulu mzuri shuleni kwa watoto
Watu wenye mkazo (stress) mara kwa mara wanakuwa na ubongo mdogo. Viwango vikubwa vya homoni cortisol (homoni ya mkazo) hupunguza ujazo wa ubongo na uwezo wa ubongo kufanya kaz
Ukiwa kwenye mahusiano imara inadaiwa Siku ya Wapendanao (Valentine's Day) ni 1 ya siku nzuri kwa afya katika mwaka. Watafiti wamedai kuwa katika mapenzi huleta faida nyingi kwa afya ya akili & mwil
Mambo yanayofanya maisha yawe ya furaha: kutunzwa vizuri na kwa upendo na wazazi kipindi cha utoto, kushirikiana na wengine wakati wa shida na raha (sherehe na misiba) & kusaidia wengine kuishi ndoto zao hasa kizazi kichanga kwa ajili ya wakati ujao mzuri (mentoring
Kwanini wazee wengine wameanza kuvuta toka wakiwa vijana na hawajapata kansa? Watafiti waligundua kuwa wavuta sigara wanaoishi hadi umri mkubwa wana chembe za urithi (jeni) maalum zinazo chochea maisha marefu.
Baadhi ya saratani husababishwa na mambo ambayo watu hufanya au kuwepo sehemu zenye hatari ya kupata saratani. Kwa mfano, matumizi ya tumbaku yanaweza kusababisha kansa ya mapafu, mdomo, koo, kibofu cha mkojo, figo, na viungo vingine vingi.
Miaka iliyopita, watu wengi ambao walikuwa na kansa hakuweza kuishi kwa muda mrefu sana. Hali hiyo imebadilika sasa. Kila mwaka watu zaidi hupona kansa na kuendelea kuishi hasa wale ambao saratani zao ziligunduliwa mapema, kabla ya kuenea.
Mtu yeyote anaweza kupata kansa katika umri wowote, lakini hatari ya kupata kansa huongezeka kadili umri unavyoongezeka. Karibia 78% ya saratani zote zimetambuliwa(kubainishwa) katika watu wa umri wa miaka 55 na zaidi
Kansa siyo ugonjwa mmoja tu. Kuna aina nyingi za saratani. Saratani inaweza kuanza katika mapafu, kifua, utumbo, au hata katika damu. Saratani ni sawa katika baadhi ya njia, lakini ni tofauti katika njia inavyokua na kuenea
Saratani inaweza kuanza sehemu yoyote katika mwili. Huanza wakati seli zikikua bila mpangilio maalumu na kushindwa kudhibitika. Hii inafanya kuwa vigumu kwa mwili kufanya kazi zake kama inavyotakiwa
Maneno Carcinos & Carcinoma yana maana ya mdudu kaa. Kaa ni mdudu wa baharini mwenye umbo bapa & miguu nane. Ugonjwa wa Kansa unafananishwa na mdudu kaa kwa kuwa unasambaa kila upande. Kaa anaweza kutembea upande wowote bila kugeuka
Asili ya neno kansa linatokana na daktari bingwa wa Ugiriki aliyeishi kati ya miaka 460 & 370 K.K aitwaye Hippocrates. Alitumia maneno 'Carcinos' & 'Carcinoma' kuelezea uvimbe unaotengeneza mchubuko na uvimbe usiotengeneza mchubuko
Kansa ni kundi la magonjwa yanayotokana na mgawanyiko usio sawa na usiodhibitika wa seli na kuunda uvimbe unaodhuru tishu. Kansa huusababishia mwili madhara pale inapoharibu seli na kuzifanya zigawanyike bila kudhibitika na kuwa uvimbe wa tishu
Magonjwa ya akili yanaweza kumfanya mtu ashindwe kabisa kutimiza majukumu yake maishani, hata hivyo watu wengi wanaougua magonjwa hayo hawapati matibabu