Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

geoffrey lea

European super league ni wazo lililotokana na mapendekezo ya viongozi wa klabu kubwa ulaya waliokuwa wanatamani kutanua wigo wa kibiashara wa mchezo wa soka hususan mashindano ya Uefa champions league...
 
MOja ya watu wa kwanza kuja na wazo hili alikuwa mkurugenzi wa Juventus Andrea Agnelli ambaye alipendekeza kuwepo kigezo cha historia kwa timu zilizofanya vizuri miaka ya nyuma kufuzu kwenye ligi ya mabingwa pale wanapokuwa wameshindwa kufuzu kwa matokeo ya uwanjani. Agnelli

1618781714113.png
 
Lengo la timu zilizoafikia kuanzisha ligi hii ni kuwepo kwa timu 15 zitakazokuwa na nafasi za kudumu kwenye ligi hii huku kukiwa na ongezeko la timu tano toka ligi kubwa 5 barani ulaya,
 
Ligi hii itakuwa kwa mfumo wa makundi mawili ya timu kumi zikicheza kwa mfumo wa nyumbani na ugenini huku mechi zikichezwa katikati ya wiki lengo likiwa kuzipishanisha na ligi za ndani
 
Jumla ya timu 12 za Ulaya (Twelve of Europe's leading football clubs) zimeridhia kuanzishwa kwa ligi hii,6 zikitoka England,Arsenal,Chelsea,Liverpool,Tottenham,Man City & Man United pamoja na 3 toka Hispania na tatu za italia zimejiunga kuunda ligi hii

Toka Hispania na Italia ni Inter na Ac Milan,Juventus,Real na Atletico Madrid pamoja na Barcelona na kama mpango huu utatimia basi ndio utakuwa mwisho wa michuano ya Uefa Champions league kama tunavyoyafahamu.
 
Kuna matarajio kwamba klabu za Ujerumani na Ufaransa zitaunga mkono wazo hili lakini Taarifa toka kwa mkurugenzi wa Borusia Dortmund Hans Joachim Watzke imethibitisha kuwa Bayern na Dortmund hawatahusika na mpango huu huku PSG wakifuata msimamo kama huo
 
Wazo hili limekuwepo muda mrefu japo Fifa na Uefa walidhani votisho walivyowahi kutoa huko nyuma vingezuia mpango lakini Andrea Agneli akamsaliti rafiki yake Aleksandr Ceferin (rais wa Uefa) na kutekeleza mpango huu saa 24 kabla ya kutangazwa kwa mabadiliko kwenye muundo wa.....UEFA CHAMPIONS LEAGUE ambayo yalikuwa yatangazwe hii leo lakini matokeo yake ni mjadala unaoendelea sasa huku mechi za UEFA zikisimamishwa kwa muda usiojulikana
 
Kinachotajwa kuwakimbiza mabosi wa klabu hizi kubwa kufikia uamuzi huu ni athari zilizoletwa na "Pandemic ya Covid19" ambapo klabu zimejikuta zikipoteza fedha nyingi na mpango huu unatazamwa kama mwokozi wa akaunti za klabu hizi ambazo tangu mwaka jana zimekuwa zinasoma hasara
 
Mabadiliko yaliyokuwa yatangazwe leo ya ligi ya mabingwa yangehusishwa ongezeko la timu 4 toka 32 mpaka 36 na ongezeko la mechi toka 125 mpaka 225 hali itakayoshuhudia ongezeko la mgao wa fedha za tv ambao unaweza kupungua kutokana na ongezeko la timu na mechi
 
Wahafidhina wa utamaduni wa michezo ya ulaya wanatumia kigezo cha uwepo wa timu 15 ambazo hazitoshuka daraja kama kigezo kikubwa cha kupinga michuano hii ambayo inakwenda kinyume na ndoto ya michel platinni ambaye alibuni mfumo unaoruhusu timu toka mataifa madogo kushiriki uefa
 
'Key players wengine wa ligi hii ukiondoa Agnelli wa Juventus ni rais wa Real Madrid Florentino Perez,wamiliki wa Manchester United Joel na Avram Glazer pamoja na mmiliki wa Liverpool John W Henry ambao hadi sasa wana uhakika wa fedha toka benki ya jp morgan ya Marekani.
 
Jp morgan ni benki ambayo ima uhusiano wa kibiashara na Familia ya Glazer na ilihusika kwenye mchakato wa familia hii kuinunua Man United Ed Woodward wa United aliwahi kufanya kazi kwenye benki hii na amekuwa sehemu muhimu ya mazungumzo kati ya benki na mabosi wa timu hizi
 
Hadi sasa msimamo wa umoja wa vilabu ulaya ECA,UEFA,FIFA na taasisi nyingine kama Premier League na hata viongozi wa siasa akiwemo Borris Johnson waziri mkuu wa Uingereza ni kupinga michuano hii kwa kauli moja,msimamo unaoonekana kufiatwa na wachezaji wengi akiwemo Ander Herrera
 
Ripoti kadhaa zinadai kuwa tayari klabu hizi kubwa 12 zimeandaa mchakato wa kisheria endapo fifa,uefa na fa zingine watafanya kweli kwenye vitisho vya kuziondoa timu hizi zinazokwenda kushiriki Uefa Super League kwenye ligi za ndani pamoja na kuwapa ban wachezaji watakaoshiriki
 
Back
Top Bottom