Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hii ilipelekea wivu na hatimaye chuki kutoka kwa jamii. Wivu huu na chuki ulisababisha tukio moja baya sana ambalo Mheshimiwa Mkapa analikumbuka kwa uchungu. Mwaka 1947, kulitokea ukame mkali, basi watu wakamleta mganga wa kienyeji akaamua kuwa mama mzazi, mama yake na bibi yake ndio walikuwa wameloga na kuzuia mvua. Walipigwa na kuteswa sana hadi Padri Mzungu alipofanikiwa kuwanasua. Bibi wa mama aliaga dunia muda mfupi baada ya tukio hilo.
 
Kijana Benjamini na mwenzie mmoja ndiyo waliopata bahati ya kuendelea na masomo ya Sekondari, kutoka darasa la watoto 25 hadi 30. Kuchaguliwa ilikuwa bahati nasibu. Shule ya sekondari ya Ndanda ilikuwa kilometa 60 kutoka Lupaso. Yeye na wenzie walitembea kwa miguu, bila viatu, kwa siku mbili, wakiwa wamebeba kichwani vitu vyao ambavyo vilikuwa vimefungwa katika mkeka. Baadae alipata sanduku la chuma.
 
Walimu wa Ndanda walikuwa wamisionari na walikazia sana sala na kazi “Ora et labora’’. Wanafunzi walipika chakula chao wenyewe. Kwa kuwa kijana Benjamini alikuwa mdogo sana alipewa kazi ya kuosha vyombo. Kawaida alivibeba vyombo kichwani mpaka mahali pa kuvioshea, na kuvirudisha. Anasema kubeba vyombo hivyo ndiyo sababu ana upara hadi leo
 
Aligombea Urais na ingawa hakushinda, wanafunzi wa kike walimpigia kura nyingi si kwa sababu alikuwa na rafiki wa kike, ila kwa jinsi alivyoweza kujieleza kuliko mpinzani wake. Alikuwa ‘More articulate!’ Aliteuliwa Makamu wa Rais wa Serikali ya wanafunzi, na hatimaye alikuwa mwenyekiti wa Baraza la wawakilishi la wanafunzi hapo Makerere
 
MAISHA NA KAZI
Simulizi ya maisha ya utu uzima iko katika sehemu mbili. Kwanza ni alipoanza kazi mpaka alipogombea Urais. Pili ni maisha ya Urais. Sehemu hii ya simulizi imejaa sifa heshima na upendo mwingi kwa Mwalimu. Anastaajabu kwa jinsi Mwalimu alivyoiunganisha nchi katika kupigania vita vya ukombozi wa bara la Africa.
 
Akiwa mtu mzima na mhitimu wa Chuo Kikuu Makerere Mheshimiwa Mkapa alipenda kuajiliwa kwenye Wizara ya mambo ya nchi za nje: Kwanza ilishindikana lakini, baadae akaambiwa, itawezekana kama ataajiriwa kwanza kama bwana shauri mkufunzi wa Wilaya, wakati akisubiri. Kwa hiyo aliajiriwa hivyo huko Dodoma April 1962.
 
Anamsifia kwa ujasiri pale alipovunja uhusiano na Uingereza. Wakati huu Mhe. Mkapa alitumia muda wake binafsi ama kusoma habari Radio Tanzania Dar es salam, ama kumchumbia Bi Anna. Siku moja aliambiwa anaitwa Msasani kwa Mwalimu. Walipaita Msasani nyumbani kwa Mwalimu “The Clinic”. Mwalimu akamwambia anamteua kuwa Mhariri Mtendaji wa gazeti la The Nationalist. Ilibidi aende Uingereza kujifunza mambo ya magazeti kwenye magazeti ya The Mirror.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…