Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Alijiunga na kuhitimu. Siku ya kuhitimu Mwalimu alikuwa ndie mgeni rasmi. Mheshimiwa Mkapa alichaguliwa na wenzie kusoma risala na Mwalimu alicheka sana alivyomtambua kuwa ni yeye kwani alikuwa amepoteza ratili nyingi za uzito. Alikuwa slim fit. Mheshimiwa Mkapa aliitwa huko β€œThe Clinic” Msasani mara kadhaa
 
April 1972 Mwalimu alimteua kuwa Mhariri Mtendaji wa Daily News
β€’ Muda mfupi baadaye Mwalimu alimteua kuwa Press Secretary wa Rais. Anasema huu ndio ulikuwa mwanzo wa maisha yake kama mwanasiasa.

β€’ Mwaka huohuo, Mwalimu alimuagiza aanzishe Shirika la Habari Tanzania – SHIHATA na kuwa Mtendaji Mkuu wake. β€’ Mwaka 1976 akamteua Balozi huko Nigeria

β€’ Mwaka mmoja baadaye akaitwa tena β€œ The Clinic” na kuteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje. Hapa alikuwa kama msaidizi wa Rais kwani Mwalimu ndiye aliyeendesha mambo ya Nchi za Nje. Alifanywa pia Mbunge wa kuteuliwa .

β€’ Aliteuliwa kuwa Balozi wa Canada 1982
 
Hakika Mwalimu ndiye shujaa mkuu wa simulizi hii. Mheshimiwa
Mkapa anamueleza Mwalimu kuwa:
β€’ Alikuwa jasiri, na kiongozi lazima awe jasiri
β€’ Alikuwa msikivu, kamwe hakumkatiza mtu hata kama alikuwa
anaeleza pumba tu.
β€’ Alikuwa mtu wa msimamo, hakuyumbayumba
β€’ Alikuwa mpatanishi na mjenga madaraja kuwaunganisha
mahasimu.
 
Mheshimiwa Mkapa anasema β€œMwalimu alikuwa mwalimu wangu kwa kila kitu”. β€’ Alikuwa mwana demokrasia mtu aliyempenda kama mrithi wake mwaka 1985 alipokataliwa na wenzie katika kamati Kuu, Mwalimu alikubali. β€’ Alikuwa kiongozi mwenye maono – visionary, alingalia maslahi na mustakabali wa Taifa ndani na nje ya mipaka yake.
 
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…