Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ni kweli ndugu tujitahidi kuonyesha wema kwa wazazi wetu
Last month nilitimiza miaka kadhaa,sasa wakati nawaza chakufanya siku hiyo,nikapata wazo la fasta kutembelea wazee wangu,maana baba ni mgonjwa wa muda na mother ndio anamuhudumia.

Sikuwapa taarifa ya ujio wangu,ila nilivyofika tu walifurahi sana,nikawashukuru kwa malezi na yote waliyofanya juu yangu na ndugu zangu.
Kiukweli ilikuwa moja ya siku ya kumbukizi kwangu maishani,kuona wanafurahia uwepo wangu na kula pamoja nao siku hiyo ya kumbukumbu. Ile furaha yao ilifungua vitu vingi sana kwangu,nashare hii kwenu ndugu zangu kuonyesha ni kwa namna gani tukiutumia muda vizuri wa wazazi tunaenjoy maisha.

Najua pia wapo ambao hawana mahusiano mazuri na wazazi wao,poleni sanaaa Mungu awajalie patano kati yenu,mfurahie kile kidogo alichowabariki pamoja nao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…