Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Chelsea wamerejesha shauku yao kwa mchezaji wa West Ham Declan Rice na wanaweza kumtumia mshambuliaji Tammy Abraham, 26, kama sehemu ya mpango wa kubadilishana. Manchester United na Manchester City wanavutiwa kumsajili Rice. (Sunday Telegraph - subscription required)
 
Leicester City ndio kilabu cha hivi karibuni kujiunga katika mbio za kumnasa beki wa Southampton na England Ryan Bertrand, na Arsenal na AC Milan pia wanahusishwa na beki huyo wa kushoto wa miaka 31, ambaye mkataba wake unamalizika msimu huu wa joto.(Talksport)
 
Juventus inaweza kuhamia kwa mshambuliaji wa Barcelona, 30, Antoine Griezmann kama mbadala wa mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo, 36, ambaye hatma yake bado iko mashakani. Juve wanafikiria uhamisho wa mkopo kwa mshambuliaji huyo wa Ufaransa, lakini pia wako wazi kwa kubadilishana na mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala, 27.(La Stampa - in Italian)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…