Mapenzi ni hisia, upendo ni imani. Mapenzi yanatawaliwa na tamaa, umiliki, ubinafsi na haja ya kupokea na kufidiwa. Upendo unatawaliwa na huruma, kujali, kusamehe, kutoa na kujitoa
The best way to retaliate is for us to publish more. If we don't pay for the angle of our story, it will always be written from the angle of another bidder.
People will hit you the most when you are down and weak. The idea to reveal your vulnerabilities in attempt to gain sympathy from people, actually it may invite them to hit you more. It is human nature. Dont be surprise when it happen. Be prepared
Epuka kulinganisha maumivu yako na ya wengine, ama kuyakadiria maumivu ya wengine. Heshimu maumivu ya watu. Maumivu hayana sare. Maumivu hayalinganishiki.
Binadamu tunatofautiana katika uwezo wetu wa kuyapokea, kuyakabili, kuyavumilia, kuyakadiria na kuyasimulia maumivu yetu. Epuka kulinganisha maumivu yako na ya wengine, ama kuyakadiria maumivu ya wengine. Heshimu maumivu ya watu. Maumivu hayana sare. Maumivu hayalinganishiki
Ujasiri uko wa namna mbili, ujasiri wa leo yako bila ya kujali kesho yako, na ujasiri wa kesho yako bila ya kufurahisha leo yako. Ni maamuzi tu ya kutafsiri nyakati kwa kipimo cha nyakati. Ukijua kupima nyakati kwa kipimo cha nyakati hutopata shida kwa nyakati zozote. PIMA
Makovu yetu hubeba taarifa muhimu za historia, huzuni, mafunzo, majuto, hasira na hata usongo wetu. Kadri tunavyoanika makovu yetu tukitafuta kujitetea, huruma na uhalali, tunawapa wabaya wetu silaha dhidi yetu. Sisi si kitu zaidi ya simulizi ya makovu yetu. Tusitiri makovu yetu.
Fanya uwezavyo katika maisha yako na hasa katika duru la watu wako wa karibu uwe na walau mtu mmoja anayeweza kukuuliza maswali magumu, machungu na usiyoyapenda.Huyu ndio mhimili wako wa kukuepusha na kufanya makosa, maamuzi mabaya na majuto huogopa sana mtu asiyewajibika kwa mtu.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.