Ipua ukwaju wako jikoni na uache kwa muda upoe andaa maji yako masafi na chujio ili uweze kuchuja juice yako kwa uangalifu zaidi ili upate juice yenyewe
Weka sukari kwa kiasi unachopendelea pia ili kupunguza ukali unaweza ukaweka hiliki au vanila ili kupata taste weka juice yako kwenye fridge ili ipoe tayari kwa kunywa.
Hizi Ndiyo Faida Kumi (10) Za Kula Ukwaju!
Unatakiwa ujaribu kuweka ukwaju karibu katika kila mlo wako kwa kila siku kwasababu ukwaju una faida nyingi kiafya ambazo hakika zitakufanya uwe na afya njema au kukuimarisha afya yako kiujumla
Ukwaju ni zao la rangi ya kahawia ambalo limefungwa na kasha gumu. Ndani ya kasha hilo kuna
vifundo vilaini ambavyo ndani yake kuna mbegu nyeusi. Vifundo hivi ndiyo ambavyo watu
wanakula ili kupata virutubisho na faida za kiafya za ukwaju.
Ukwaju una ladha fulani ya uchachu ukiwa bado mchanga, lakini kadiri unavyozidi kukomaa unakuwa na ladha tamu. Ingawa ukwaju unakuwa na utamu kadiri unavyokuwa na kukomaa, kiujumla ukwaju ni mchachu.