Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

20210604_115908.jpg
😁
 
Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru!
Mlango wa Kwanza
Siri Nzito

Mtawaliwa siku zote anataka kumuigiza mtawala katika maumbile yake, mavazi yake, kazi zake na yote yanayokhusiana na hali yake na dasturi zake.
—Ibn Khaldun


Mapinduzi Tanganyika na Kenya Picha kubwa ya Mapinduzi ya Zanzibar ya 1964 haiwezi kufahamika bila ya kuyafahamu ijapokuwa kwa mukhtasari mfupi mapinduzi ya kabla yake yaliofanyika Tanganyika, na baadaye Kenya. Mapinduzi ya Tanganyika, ya Zanzibar, na ya Mwambao wa Kenya ni mifano ya mapinduzi ya kalamu na ya umwagaji damu.
 
Tanganyika iliupata uhuru wake tarehe 9 Disemba 1961 na Waislam wa Tanganyika walikuwa na mchango mkubwa sana katika kuupiganiya uhuru huo. Hayati Julius Kambarage Nyerere alitowa mchango mkubwa na yeye mwenyewe alikiri hivyo kwenye hotuba yake ya kuwaaga wazee aliyoitowa Dar es Salaam katika mwezi wa Novemba mwaka 1985. Kwa mara ya kwanza Mwalimu alielezeya namna alivyopokelewa, kujuulishwa na kusaidiwa sana na wazee wa Kiislamu wa Dar es Salaam. Kwenye shughuli za TANU yeye alikuwa ni Mkristo peke yake na mara nyingine alikuwepo John Rupia.
 
Muhimu pia na kwa mara ya kwanza Mwalimu alisikika akisema kwenye hotuba hiyo kuwa hata jina la Tanganyika African National Union (TANU) lilifikiriwa na kuundwa na akina marehemu Abdulwahid Sykes walipokuwa askari Burma katika vita vya pili vya dunia Historia iliyofichwa ya mchango wa Waislam katika kuupiganiya uhuru wa Tanganyika imeandikwa na kuelezwa kwa ufasaha mkubwa na mwandishi maarufu wa Tanzania Bwana Mohamed Said kwenye kitabu chake kwa lugha ya Kiingereza,

The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924–1968), na kwa Kiswahili Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924–1968) Historia Iliyofichwa Kuhusu Harakati za Waislam Dhidi ya Ukoloni wa Waingereza katika Tanganyika. Kitabu hicho ni muhimu sana kwa wanaotaka kufahamu vipi Waislam waliupiganiya uhuru wa Tanganyika na namna walivyopinduliwa kwa mapinduzi baridi kwanza kabla ya kupinduliwa kwa Dola ya Zanzibar tarehe 12 Januari 1964.

Kilele cha mapinduzi ya Tanganyika ni kudhoofishwa nguvu za umma wa Kiislamu pale ilipovunjwa East African Welfare Muslim Society (EAMWS) na zilipozimwa juhudi za kuanzisha Chuo Kikuu cha Kiislam mwaka 1964.
 
Bwana Mohamed Said pia amefafanuwa katika kitabu chake Uamuzi wa busara wa Tabora namna gani uongozi wa Waislam kutokeya African Association mpaka kuundwa kwa TANU walivyopinduliwa kwa mapinduzi ya kalamu. Baraza la Wazee la TANU ambalo Mwenyekiti wake alikuwa marehemu Mzee Suleiman Takadiri lilipinduliwa chali kwa kazi iliofanywa na kiongozi na viongozi wa Kiislam waliouweka mbele uzalendo wa Kiafrika kuliko mafundisho ya dini yao. Chanzo cha mapinduzi hayo yalikuwa masharti matatu yalioikabili TANU katika kushiriki uchaguzi wa kwanza wa Tanganyika wa kulichaguwa Baraza la Kutunga Sheria
 
Mkutano wa TANU wa Tabora wa tarehe 21–26 Januari 1958 uliamua kuingiya uchaguzi wa kibaguzi wa kura tatu ambao ulikuwa na masharti matatu magumu:
1) Ili Mwafrika aweze kupiga kura alitakiwa awe na kipato cha pauni mia nne za Kiingereza kwa mwaka.
2) Awe na kiwango cha elimu ya darasa la kumi na mbili.
3) Na awe ameajiriwa katika kazi maalumu.

Uamuzi wa busara wa Tabora haukuwanasa Waingereza kama ulivyowanasa Waislam wa Tanganyika ambao wengi wao hawakuweza kuwachaguwa viongozi wao kwa sababu uchaguzi wa kura tatu “ulikuwa ukizuia uongozi wa kuchaguliwa kuingia kwenye madaraka.”
 
Kwa upande mwengine, Kenya kabla ya kupata uhuru wake tarehe 12 Disemba 1963, siku mbili baada ya uhuru wa Zanzibar, ilikuwa imegawanyika sehemu mbili: Koloni la Kenya, au bara, na Himaya ya Kenya, au Mwambao. Sheikh Abdillahi Nassir ni mmoja kati ya viongozi wa Mwambao ambaye alihudhuriya mkutano wa Mwambao uliofanyika Lancaster House, London, baina ya tarehe 8–12 Machi mwaka 1962.

Anaelezeya Sheikh Abdillahi kwenye kanda iitwayo “Mwambao: Historia ya Pwani ya Afrika Mashariki,” kuwa Himaya ya Kenya ilikuwa ni nchi kabla ya Koloni la Kenya kuwa ni nchi kwa miaka isiyopunguwa 1,300, na namna chuki za uzalendo wa Kiafrika zilivyowaathiri Waislam na khasa chuki za kikabila na propaganda ya utumwa na Uarabu

Sehemu hizo mbili za Kenya, Koloni la Kenya na Himaya ya Kenya au Mwambao, zikawa ni nchi moja ya Kenya kwa makubaliyano ya mabadilishano ya barua baina ya Waziri Mkuu wa Kenya, Mzee Jomo Kenyata na Waziri Mkuu wa Zanzibar Bwana Mohammed Shamte walizoandikiyana London tarehe 5 Oktoba 1963.
 
Barua zote mbili zilikubaliyana juu ya mambo matano yafuatayo:
1) Uhuru wa kuabudu wa watu wa dini zote katika sehemu hiyo utalindwa kwa mujibu wa dini zao; na khasa wale raia wa Sultani na vizazi vyao, ambao ni wa dini ya Kiislamu, watahakikishiwa uhuru wao wa kuabudu katika nyakati zote na hifadhi za nyumba na sehemu zote za dini yao.
2) Uwezo wa Kadhi Mkuu na Makadhi wengine wote kuhukumu kwa sharia ya Kiislamu utahifadhiwa kufuatana na sharia ya Kiislamu katika kesi zote za ndoa, talaka na mirathi.
3) Katika zile sehemu ambazo wakaazi wake wengi ni Waislamu, watawekwa, kila inapowezekana, Maafisa Utawala (Mabwana Shauri) Waislamu.
4) Watoto wa Kiislamu, kwa kadri inavyowezekana watasomeshwa lugha ya Kiarabu katika kudumisha dini yao ya Kiislamu kwa vile lugha hii ndiyo lugha ya dini yao. Ule msaada wa fedha unaotolewa kuzisaidia skuli za msingi za Kiislamu katika hilo jimbo la Mkoa wa Pwani utaendelea. Hautakatwa.
5) Umilikaji wa ardhi kutokana na mikataba iliyokwisha kusajiliwa utatambulikana na kukubalika wakati wote. Mwenendo huohuo utaendelea na kuhifadhiwa katika kusajili mikataba mipya ya kumiliki ardhi isipokuwa tu pale itakapokuwa ni lazima kuchukua ardhi kwa masilahi na faida ya umma; lakini papo hapo wale wenye ardhi zao watabidi kulipwa fedha
 
Kwa mujibu wa Sheikh Abdillahi, makubaliano hayo baina ya Serikali ya Zanzibar na Serikali ya Kenya hayakutimizwa na amethibitisha namna nguvu za umma zilivyoporwa na umuhimu wa kujenga muamko wa kuelewa badala ya muamko wa hamasa. Mfano mkubwa ambao ameutowa Sheikh Abdillahi ambao ni kinyume na makubaliano waliyotiya sahihi Mawaziri Wakuu wa Zanzibar na wa Kenya, ni kunyanganywa Waislam, wa makabila yote,

Taasisi muhimu sana ambayo ikijulikana kwa jina maarufu la Mombasa Insititute of Muslim Education (MIOME) ambayo ilikuwa ni:
baraka kubwa kwa Waislam wa Afrika Mashariki. Hapa ndipo mustakbal wa vizazi vya Waislam vinapewa mafundisho katika masomo ya ufundi chini ya Maprofesa mabingwa ambao wameajiriwa na Serikali kutoka Ulaya. Sir Phillip Mitchell ambaye alikuwa ni Gavana na sasa ni Mwenyekiti wa Baraza la Waendeshaji wa Taasisi alikuwa ndiyo nguvu ya usukumaji wa Taasisi [MIOME]. Mtukufu Sultan wa Zanzibar alitowa mchango wa Shs. 2,000,000/- kutoka mfuko wa Colonial Welfare Fund, Mtukufu Aga Khan alichangiya Shs. 2,000,000/-: Mtukufu Sheikh Mkuu wa jamii ya Kibohora amechangiya Shs. 1,000,000/-; na Sheikh Khamis Mohammed bin Juma [El Mutwaji] amekodisha ekari 34 na nusu za ardhi nzuri na kwa muda mrefu kwa matumizi ya Taasisi, na kwa bei khafifu kwa kila mwaka.
 
Mbali ya Muslim Teachers’ Training College iliyokuwepo Kibuli, Kampala, Uganda, Khamisi Sekondari ya Mombasa, Muslim School ya Soroti, ya Jinja, na kadhalika. Iliyovunja rekodi zote na ambayo marehemu Sheikh Ali Muhsin akiamini kuwa ndiyo moja kati ya sababu za kupinduliwa Zanzibar, ilikuwa ni fikra na mipango ya kuanzisha Chuo Kikuu Cha Kiislam cha Afrika Mashariki na Kati.

Kwa mujibu wa Sheikh Ali Muhsin, Chuo hicho kilikuwa na lengo la kuwafundisha Waislam kutoka sehemu zote za Afrika Mashariki na Kati. Mwandishi wa ramani wa Chuo hicho alikuwepo Zanzibar mapinduzi yalipotokeya na alisaidiwa kuondoka na Bwana Ahmed Omar Jahadhmy. Wamasri waliishauri serikali ya Zanzibar wasubiri mpaka watakapokuwa na wanafunzi wa kutosha ambao wataweza kufundishwa kwenye Chuo hicho.

Fikra iliyoona mbali kwa wakati huo ni hii ambayo leo inaitwa Open University. Redio na televisheni vilikuwa viwe ndiyo vyombo viwiili vikubwa vya kufundishiya kote Afrika Mashariki na Kati. Majaribio ya kwanza yalifanywa kabla ya mapinduzi lakini yalifeli
 
Baada ya kuvunjwa kwa East African Muslim Welfare Society ambazo khabari zake zinapatikana kwa urefu kwenye kitabu cha Kiswahili cha Bwana Mohamed Said cha Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes, taasisi na mali zake zote zikataifishwa na badala yake pakaundwa BAKWATA Tanzania, SUPKEM Kenya na UMSC Uganda. Hali ya Waislam chini ya utawala wa Kiingereza ilikuwa ni ya kuridhisha zaidi kuliko hali waliyokuwa nayo baada ya kupatikana uhuru Tanganyika, Kenya na hata Uganda.
 
Waingereza Walijuwa Nini Kuhusu Mapinduzi?
Ukiangaliya kwa makini utakuja kuona kuwa walikuwepo Waingereza na mamishionari ambao walikuwa hawana chuki dhidi ya Wazanzibari wenye asili ya Kiarabu lakini kwa bahati mbaya sauti zao sio zilizokuwa zikisikilizwa na kupewa nafasi.

Kwa mfano alikuwepo Dk. Gerald Broomfield ambaye alikuwa ni mmishionari wa Kianglikani aliyekuwa na uzowefu mkubwa Zanzibar. Dk. Broomfield alinukuliwa na Arab Association ya Zanzibar kutoka kitabu chake Colour Conflict in Africa kwa maneno yake yafuatayo:

Afrika iliyobakiya ina jambo la kujifunza kutoka Zanzibar…Zanzibar inaonyesha uwezekano wa kuwepo amani na kuhishimiana baina ya makabila. Huenda likawa ni jambo zuri kwa roho zetu kukumbuka [Zanzibar] inafanya hivyo kwa sababu Sultan wa Kiarabu ndiye mkubwa wa Dola
 
Hilo halistaajabishi kwa sababu Ukristo uliingiya Zanzibar na bara kwa kupewa hishma na Masultani waliokuwa ni Waarabu na Waislamu. Lakini Muingereza mtawala alipoona kuwa Ufalme umegeuka na kuiunga mkono siasa ya kizalendo ya chama cha Zanzibar Nationalist Party (ZNP) ambayo ilikuwa karibu sana na siasa ya uzalendo wa Kiarabu (Pan-Arabism au Arab Nationalism) wa Gamal Abdel Nasser wa Misri, akaamua kuwatupa mkono ZNP-ZPPP na kuubwaga uhuru wa Zanzibar ambao ulikuwa hauna salama kwa Waingereza au kwa Mwalimu Nyerere kwa sababu, na kama alivyoelezeya Sheikh Abdillahi:

Zanzibar ilikuwa ni nchi pekee katika Afrika nzima ambayo isingelihitajiya Mzungu hata mmoja. Zanzibar ilikuwa ina watu wa kuendesha nchi na kuwaazima majirani kuendesha nchi zao
 
Sababu kubwa ya Wazanzibari wenye asili ya Kiarabu kuwageuka watawala wa Kiingereza na watawala hao kupanga kuwakomowa Wazanzibari wenye asili ya Kiarabu, kulianza kwa kupigwa mabomu Misri na Muingereza mwaka 1956. 11 Wazanzibari wenye asili ya Kiarabu walihisi kuwa Uingereza haiaminiki na kuwa ilikuwa dhidi ya Waarabu. Hisia hii ilisababisha kudai uhuru kamili bila ya kungojea maendeleo zaidi ya baadae.

Mwisho wa mivutano Muingereza alikataa kuisaidiya serikali ya Zanzibar ilipopinduliwa tarehe 12 Januari 1964 na sababu kubwa iliyowafanya kukataa ni imani yao kuwa Mapinduzi ya Zanzibar yalikuwa ni suala la ndani ya Zanzibar na kuwa hakukuwa na mkono au uvamizi kutoka nje ya Zanzibar.

Kwa upande wa Tanganyika Muingereza aliamuwa kuzuwiya fujo na kumrejesha kitini Mwalimu Nyerere pale jeshi la Tanganyika lilipoasi tarehe 20 Januari 1964 na Nyerere akakimbilia mafichoni siku tisa tu baada ya mapinduzi ya Zanzibar.
 
Back
Top Bottom