Kamati ya Ukombozi wa Afrika
Mkutano wa nchi huru za Kiafrika uliofanyika Addis Ababa mwezi wa Mei 1963 uliunda Kamati ya Ukombozi wa nchi tisa yenye makao makuu Dar es Salaam. Nchi zilizounda kamati hiyo zilikuwa Tanganyika, Nigeria, Uganda, Algeria, Umoja wa Jamhuri ya Kiarabu (U.A.R.), Guinea, Senegal, Ethiopia na Kongo. Ghana haikuwemo.
Nyerere hakupendeleya makao makuu ya Kamati ya Ukombozi ichukuliwe na Ghana, U.A.R. au Algeria. “Alikhofiya kuwa kati ya nchi hizo Kamati ingelitumiliwa na Rais wa Dola kujijengeya sifa, na mtizamo wa kamati ungelikuwa juu ya utumiaji nguvu badala ya shinikizo la amani.”