Bara la Afrika ndio bara pekee duniani liloweza kubarikiwa kuwa na wanyama wa tano wakubwa wa porini.
Wanyama hawa hawakuchanguliwa kwakuangalia ukubwa wa miili yao ila nikutokana ugumu wa kuwindwa na pia ndio wanyama hatari na wenye hasira kali kuliko wote. Wanyama hao ni pamoja na Tembo, Faru, Nyati , Simba na Chui.
Nchi pekee barani Afrika ambazo wanyama hawa wakubwa wa tano hupatikana ni pamoja na nchi ya Tanzania, Botswana, Zambia, Uganda, Namibia, Ethiopia, Afrika ya Kusini, Kenya, Zimbambwe, Kongo, na Malawi.
Tembo ndio mamalia mkubwa kuliko wote dunia, huwa na ngozi isiyona na vinyoleo, meno marefu na yaliotokeza kwe nje. Kuna spishi mbili za tembo moja ni tembo wapatikanao katika misitu na pia tembo wapatikanao katika vichaka. Tembo huishi katika familia ya makundi isiyo pungua tembo mia moja huku kiongozi wa familia akiwa ni tembo jike.
Faru ni mamalia wa pili kwa ukubwa baada ya tembo, huku kukiwa na spishi mbili za faru wapatikanao barani Afrika ambazo ni faru mweupe na faru mweusi. Utofauti ya faru hawa ni kwenye namna ya midomo yao ilivyo kaa na sio rangi kama wengi wananyodhani.
Kwa bahati mbaya hivi sasa wanyama hao wamekuwa wakipungua kutokana na ongezeko la ujangili uliokithiri barani Afrika. Pembe ya faru inasadikika kutumika kama tiba ya magongwa mbalimbali hasa bara la Asia.
Nyati dume hukuwa na kufika futi 4-6 na kilo 700, nyati amehesabika kupoteza maisha ya watu wengi kuzidi wanyama wengine wa porini. Ni mnyama mwenye hasira kali sana na pia ni hatari sana.
Simba ndio paka mkubwa kati ya wapatikano bara la Afrika. Dume huwa na manyoya kuanzia kwenye mabega yake nakuelekea kwenye kichwa chake. Simba huweza kuishi hadi miaka kumi na nane akiwa porini, lakini wengi wao hupoteza maisha kutokana na kupingana kati ya wenyewe kwa wenyewe.
Ni moja kati ya paka wakubwa watano wapatikanao porini ila imekuwa vigumu sana kumuona chui hata ukiwa porini nikutokana na mazingira ambayo amekuwa akishi. Chui upendelea kuishi juu ya miti na kutumia mazingira hayo kama njia yake ya kujilinda.
Zipo sababu nyingi zimetajwa kuwa zinaweza kumfanya mtu aishi kwa furaha ambazo ni pamoja na kumuamini Muumba wako; Kuwa na upendo kwa ndugu na jamaa, kudumisha amani ya moyo wako, huku ikitajwa furaha hiyo kuwa ni moja ya sababu zinazoweza kukufanya uwe na afya nzuri.
Leo nimekutana na hii ya njia sita ambazo furaha inaweza kuimarisha afya yako.
Furaha huulinda moyo wako,
-Utafiti unaonesha kuwa asili ya upendo na furaha siyo moyoni lakini husaidia kuulinda huku ikibainika kuwepo kwa uhusiano baina ya furaha na vipimo vingine vya afya ya moyo kama vile muda unaotumika wakati wa pigo moja la moyo na lingine na kuzilinganisha na hatari kadhaa za magonjwa ya moyo.
Furaha huimarisha mfumo wa kinga mwilini
-Utafiti unaonesha kuwa mfumo wa kinga ya mwili hupanda na kushuka kutegemea na furaha aliyokuwa nayo mtu ambapo kuna uhusiano mkubwa baina ya furaha na mfumo imara wa kinga.
Furaha huzuia mkazo (stress)
-Mkazo (stress) hausababishi matatizo ya kisaikolojia pekee bali pia husababisha mabadiliko ya ki-biology katika homoni zetu na shinikizo la damu. Furaha inatajwa kupoza hasira za athari hizi na wakati mwingine kutusaidia kurudi katika hali ya kawaida kwa haraka.
Watu wenye furaha hawaumwi mara kwa mara na huwa na kiwango kidogo cha maumivu
-Watu ambao wana mood nzuri wana nafasi nzuri sana ya kuimarisha furaha ambayo huwasaidia kutoumwa homa za mara kwa mara na huwa na kiwango kidogo cha maumivu tofauti na watu ambao wana mood mbaya.
Furaha hurefusha maisha
-Watu wenye furaha huweza kuishi kwa miaka 7-10 zaidi tofauti na wasiokuwa na furaha. Katika utafiti uliofanywa kwa wazee 4,000 wa Uingereza wenye umri wa miaka 52-79 ambao walikuwa na furaha mara nyingi zaidi kwa siku na kuonesha kuwa watu wenye furaha.
Imeandikwa pendaneni kama nilivyo wapenda ninyi. Visababishi vya msongo wa mawazo nyakati hizi ni vingi. Kwakua upendo wa wanadamu sasa uko chini ya kiwango kisicho faa. Wengi wetu wanasema tunampenda Mungu, hapohapo wanamchukia mwanadamu wenzao.. Mambo yanayosababisha msongo wa mawazo ni mengi. Na msongo wa mawazo huleta madhara mengi mwilini. Furaha, Upendo na kujaliana sisi kwa sisi, huongeza umri wa kuishi nk