Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ukilinganisha virutubisho vilivyomo kwenye jamii zote za mtama, ukalinganisha na wali, mahindi, ngano vyote hivi vinaachwa mbali mbali mbali sana!

Iwe ni nyuzilishe hata antioxidants (uwezo wa kupambana na kemikali zururaji mwilini). Hiki ndio chakula sasa.
 
Ulezi una madini ya kalsimu kuliko nafaka zingine zote. Yaani kwenye gram 100 za ulezi unapata kalsimu mg 350. Anayemfuatia hapo ni uwele ambaye ana gm 42 kwenye gram 100. Wengine ndio basi tena. Kwa kiwango hiki hata maziwa hayagusi, ulezi upo juu!
 
Ukizungumzia madini ya chuma uwele unafanya vizuri kuliko ulezi. Utaona kumbe hakuna nafaka moja yenye kila kitu, nafaka hii ina hiki zaidi kuliko wengine na nyingine ina kitu kingine kizuri kuliko zingine. Kwahiyo ni vizuri kuzichanganya au kula kila mmoja kwa wakati bila kuidharau.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…