Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Wanaume waliojihami wamewaua karibu watu 100 katika shambulio dhidi ya kijiji kimoja kaskazini mwa Burkina Faso, Rais Roch Kabore amesema.

Wakati wa shambulio hilo la usiku dhidi ya Solhan, nyumba na soko pia ziliteketezwa, shirika la habari la Reuters linanukuu taarifa ya serikali.

Hakuna kundi lolote lilitangaza kuhusika na shambulio hilo.

Lakini mashambulio kutoka wanamgambo wa Kiislamu yameongezeka nchini humo, hasa maeneo yanayopakana na Niger na Mali.
 
Rais Kabore ametangaza siku tatu za maombolezu ya kitaifa akisema, katika ujumbe wa Twitter, kwamba "lazima tuungane dhidi ya maadui".

Vikosi vya usalama kwa sasa vinawatatfuta waliohusika shambulio hilo, aliongoza.

Katika shambulio lingine la usiku wa Ijumaa, watu 14 waliripotiwa kuuawa katika kijiji kingine, karibu kilomita 150 kaskazini mwa Solhan.

Mwezi uliyopita, watu 30 walifariki katika shambulio mashariki mwa Burkina Faso.

Nchi hiyo inakabiliwa na mzozo mkubwa wa usalama, sawa na majirani zake, kwani makundi yaliojihami yanashambulia na kuwateka katika eneo hilo.
 
Mnamo mwezi Mei, jeshi la Burkina Faso lilizindua oparesheni kubwa ya kudhibiti mashambulio ya wanamgambo.

Licha ya hatua hiyo, vikosi vya usalama bado vinajizatiti kuzuia ghasia ambazo zimesababisha zaidi ya watu milioni moja kutoroka makwao katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.

Mataifa kadhaa masikini zaidi duniani yanapakana na jangwa la Sahara.

Ukanda huo unajulikana kama "Sahel", neno la Kiarabu linalomaanisha "pwani".

Mali, Chad, Niger, Burkina Faso na Mauritania zinaunda nchi za Sahel na zote zimepata mashambulio kutoka kwa wanamgambo.

Sehemu za ukanda huo zinakumbwa na ukame, umaskini, ukosefu wa ajira na ufisadi.
 
Kiungo wa kati wa Aston Villa na England Jack Grealish, 25, huenda akasalia katika klabu hiyo msimu huu wa joto, baada ya Manchester City na Manchester United kushindwa kufikia bei ya Villa ya £130m, kulingana na nahodha wa zamani wa Villa Gabriel Agbonlahor. (Talksport
 
Kiungo wa kati wa Manchester City na Brazil Fernandinho, 36, na mshambuliaji wa Newcastle na England Andy Carroll, 32, wamejumuishwa katika orodha ya klabu zao za wachezaji watakaoondoka ambayo ilichapishwa na Ligi ya Primia. Hata hivyo klabu zina hadi tarehe 23 Juni kutuma orodha zao mwisho.. (Premier League)
 
Kiungo wa kati wa Manchester City na Brazil Fernandinho, 36, na mshambuliaji wa Newcastle na England Andy Carroll, 32, wamejumuishwa katika orodha ya klabu zao za wachezaji watakaoondoka ambayo ilichapishwa na Ligi ya Primia. Hata hivyo klabu zina hadi tarehe 23 Juni kutuma orodha zao mwisho.. (Premier League)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…