Kuhusu fidia na namna ya kushughulikia ajali kama hiyo, kuna mikataba miwili ya kimataifa ambayo ilipitishwa mwaka 1967 na mwaka 1972 ambayo inatoa muongozo wa nini cha kufanyika.
Mkataba wa mwaka 1972 ni juu ya dhima za nchi ambazo zinafanya shughuli katika anga za mbali pale endapo kuna jambo lolote litatokea kupitia vifaa vyake.
Nchi mbalimbali za Ulaya, Marekani na hata China zimetia saini mkataba huo. Na kukubali dhima haimaanishi kuwa nchi imevunja sheria, bali inatambua wajibu wake wa kimaadili kwa kile kilichotokea na ipo tayari kushughulika janga ama ajali hiyo.
Mwaka 1978, satelaiti ya Usovieti Kosmos 954 ilipata hitilafu ikiwa katika anga za juu na mabaki yake kuangukia katika eneo la kaskazini magharibi ya Canada, na kusambaza taka za sumu ardhini.
Awali Usovieti ilijaribu kukanusha kuwa satelaiti hiyo haikuwa yao lakini baada ya majadiliano wakakubali kulipa Dola milioni 6 za Canada. Hakuna ushahidi kama kiasi hicho kililipwa chote.
Hofu ya kuanguka kwa vyombo vingine vilivyopo angani sasa itazidishwa na ufichuzi huo kwamba kunavyo vingine 200 ambavyo wakati wowote vinaweza kugongwa na kuanguka vikiwa vipande au hata kugonga setilaiti muhimu kwa shughuli na maishaya binadamu katika sayari yetu .