Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Baada ya ugunduzi wa Albert von Szent na haworth wakaipa herufi C kemikali iitwayo ascobic acid. Na hii ndiyo vitamini C. hivyo herufi C kwenye vitamini C ina maana ascobic acid hii ni tindikali. Wataalamu wa afya wanatueleza kuwa wanyama katu hawawezi kuishi bila ya vitamini C mwilini mwao.Vitamini C ndio vitamini vya kwanza kuweza kutengenezwa na binadamu kikemikali.
 
VYAKULA VYA VITAMINI CKwa kuwa tumeshajuwa sasa maana na historia ya vitamini C hapa nitakwenda kukueleza chanzo cha vitamini C na je ni katika vyakula vipi tunapata vitamini C. kwa ufupi wa somo ni kuwa vitamini C unaweza kuvipata kwenye matunda yenye ladha ya uchachu uchachu (citrus) na matunda vyenye rangi ya njano na kwenye mboga za majani
 
Tofauti na mboga za majani na matunda ya uchachu na yenye rangi ya njano pia tunaweza kupata vitamini C kwa kula maini, maziwa na mayai. Pia unaweza kupata vitamini C kwa kumezaa vidonge vya vitamini C.
 
KAZI ZA VITAMINI C MWILINI

Kama tulivyowkisha kuona kuwa vitamini C hulunda mwili dhidi ya mashambulizi na sumu za vyakula. Pia basi vitamini C husaidia katika kulinda mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali kma kiseyeye, magonjwa ya ngozi, mifupa na moyo. Katika kipengele hiki utakwenda kuona kwa undani zaidi kuhusu kazi hizi za vitamini c mwilini:
 
Kazi kuu tatu za vitamini C

1.Husaidia katika utengenezwaji wa collagen hizi ni protini ambazo huhusika katika utengenezwaji wa tishu kitaalamu zinazotambulika kama connective tissue na pia husaidia katika uponaji wa vidonda na majeraha. Mtu mwenye upungufu wa vitamini C vidonda vyake vitachelewa sana kupona ukilinganisha na mwenye vitamini C vya kuatosha.
 
Tishu hizi ndizo ambazo zilitupa umbo letu, kwa lugha nyepesi hizi nyama zinazoonekana kwenye miili yetu, zilizofunika mbavu, mifupa, magoti, kichwa na maeneo yote ya mwili. Tishu hizi pia zinapatikana kwenye viungio vya miili yetu. Mifupa laini ya kwenye viungio vyetu pia ni katika tishu hizi. Hivyo protini huhusika katika utengenezwaji wa hizi tishu.
 
Vitamini C ni antioxidant katika miili yetu antioxidanti hufanyakazi ya kulinda miili dhidi ya mipambano ya kikemikali ya melecule ndani ya miili yetu.. Antioxidant ni chembechembe za kikemikali ambazo husaidia katika uuguzwaji wa oksijeni mwilini. Husaidia kuzui antioxidant hupunguza sumu za vyakula wilini.
 
 
Miili yetu inahitaji antioxidant ili iweze kujilinda na kuwa madhubuti. Zipo antioxidant nyingia mbazo tunaweza kuzipata kwa vyakula. Mifano hiyo ni:-
Caroteese ambayo tunaweza kuipata kwenye karot.
Vitamini E
Vitamini C
uric acid
 
Kazi nyingine za vitamini C
1.Hulinda mwili dhidi ya maradhi ya kiseyeye (scurvy):
Ugonjwa wa kiseyeye husababishwa na upungufu wa vitamini C na kutibiwa kwa kupata vitamini C aidha kwa kutumia vyakula ama vidonge vya vitamini C. dalili za ugonjwa huu huanza kutokea mwezi mmoja toka upungufu wa vitamini C uanze kutokea mwilini.
 
Dalili za ugonjwa wa kiseyeye:
1.Kushindwa kuhema vizuri
2.Maumivu ya mifupa
3.Mafinzi kutoka damu
4.Uponaji ulio hafifu wa vidonda
5.Homa
6.Mwili kukosa nguvu
7.Maumivu ya misuli na viungio
8.Kifo
 
Kulinda mwili dhidi ya maambukizi na mashambulizi:
Tafiti mbalimbali zilizofanya zinaonesha kuwa vitamini C inaweza kusaidia kupunguza nguvu za virusi waletao mafua na homa ya mafua. Baadhi ya tafiti zinadiriki kusema kuwa vitamini hivi kuponyesha mafua yaa kwa haraka, lakini ambalo halina shaka ni kuwa vitamini c vinaweza kupunguza kupata mafua ya mara kwa mara au kufanya mafua yaondoke kwa haraka.
 
Vitamini C ni muhimu sana katika mfumo wa kinga mwilini. Kwani vitamini C husaidia katika Antimicrobial yaani katika kuzuia vijidudu shambulizi mwilini kama bakteria na virusi, pia vitamini C husaidia katika Natural killer cell yaani katika kuuwa vijidudu shambulizi ama kuvizuia visiendelee kukua mwilini, pia vitamini C husaidia katika kuimarisha mfumo wa kinga kwa kuimarisha seli hai nyeupe ziitwazo lymphocyte hizi ndizo seli ambazo askari mkuu wa mwili dhidi ya vimelea vya maradhi kama virisi, fangasi, protozoa na bakteria.
 
Kulinda miili yetu dhidi ya saratani (cancer):
Tafiti mbalimbali zimefanywa kuhusu aina ya saratani na zinavyohusiana na vitamini C kama saratani ya matiti na mapafu. Ijapokuwa tafiti hizi hazikuweza kuthibitisha moja kwa moja kuwa vitamini C vinasaidia kuondoa saratani hizi kalaki kuna mambo ambayo tafiti hizi yametufungua mawazo:
A.Vitamini C husaidia kuborsha afya na kuishi vyema kwa wagonjwa wa saratani
B.Vitamini C inaweza kuuwa seli zinazotengeneza uvimbe wa saratani
 
UPUNGUFU WA VITAMINI C
Endapo kutatokea upungufu wa vitamini C mwilini kuna athari kubwa itakayotokea mwilini ikiwemo:
Kupata ugonjwa wa kiseyeye
Kuchelewa kupona kwa vidonda
Kutokwa na damu kwenye mafinzi
Maumivu ya mifupa
Maumivu ya misuli na viungio
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…