Kiungo wa kati wa RB Leipzig raia wa Austria Marcel Sabitzer, 27,ambaye awali alihusishwa na tetesi za kuhamia Tottenham, anataka kuondoka klabu hiyo ya Bundesliga na huenda akanunuliwa kwa karibu euro milioni 15 msimu huu. (Athletic, subscription required)
West Ham wameongeza juhudi za kumsajili Jesse Lingard kwa mkataba wa kudumu kutoka Manchester United baada ya kiungo huyo wa kati wa Uingereza kutemwa katika kikosi michuano ya Ulaya. (Sun)
Porto wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kumsaini kiungo wa kati wa Liverpool na Serbia Marko Grujic baada ya kuwa katika klabu hiyo msimu uliopita kwa mkopo. Porto hata hivyo inakabiliwa na upinzani kutoka klabu za Ujerumani na Italia ambazo pia zinawania saini ya nyota huyo wa miaka 25. (Athletic, subscription required)
Kocha wa Roma Jose Mourinho amewasiliana na mshambulizi wa Torino na Italia Andrea Belotti, 27, ambaye anaongoza orodha ya wachezaji anaotaka kuwasajili. (Goal - in Italian
Deportivo Alaves wanataka kusaini mpya mkataba wa mkopo wa winga wa Manchester United na Uruguay Facundo Pellistri,19. (Noticias de Alava - in Spanish)