Kinywaji cha Fanta kilianza kutengenezwa rasmi nchini Ujerumani kipindi cha Vita Ya Pili Ya Dunia (WW2) hasa kutokana na changamoto za upatikanaji wa kinywaji cha Coca-Cola, Hivyo Fanta ilikua ni kama mbadala wa Coca-Cola
Fisi wana akili kuliko Sokwe, Tafiti kadhaa zimeonesha kua Fisi wana uwezo mkubwa wa kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili (Wanajiongeza) kuliko wanyama wengine kama Sokwe.
Auckland, New Zealand, imetajwa kuwa ndio miji bora zaidi kwa mtu kuishi duniani katika wakati huu wa janga la virusi vya Corona.
Tathmini ya miji bora iliyofanywa na kitengo cha masuala ya uchumi -Economic Exploration Unit (EIU), iliangazia miji 140 ikizingatia masuala kama vile utulivu, elimu na upatikanaji wa huduma za afya.
Hatahivyo janga la virusi vya corona limekuwa kigezo kikuu katika tathmini ya miji ya mwaka huu na jinsi majukumu yanavyogawanywa
Katika tathmini hiyo Ulaya imeonekana kushuka katika kiwango chake cha awali huku miji ya Australia na Japan pamoja na New Zealand ikipanda zaidi kwenye nafasi bora.
Mataifa haya yaliyoko katika maeneo ya theluji yalishughulikia haraka mlipuko wa virusi vya corona na yaliweza kupunguza idadi ya watu wanaoambukizwa na kulegeza masharti ya kudhibiti maambukizi ya virusi hivyo.
Mataifa ya Muungano wa Ulaya, wakati huo huo, yalichelewa kuanza kutoa chanjo, na mataifa mengi ya Ulaya yaliweka masharti makali ambayo yameifanya miji hiyo kufanya vibaya katika utafiti wa mwaka huu wa miji bora zaidi ya kuishi duniani.
Kupanda kwa mji wa Auckland kumetokana na kufanikiwa kwa mbinu yake ya kukabiliana na Covid-19, ambapo iliruhusu watu kuwa wazi zaidi kuhusu janga hilo na mji ulikuwa na mchango bora katika kuzuia maambukizi ," ilisema taarifa ya EIU.
"Miji ya Ulaya imefanya vibaya sana katika orodha ya mwaka huu ya miji bora ya kuishi," aliongeza.
Orodha ya miji bora zaidi kuishi ni
Auckland, New Zealand
Osaka, Japan
Adelaide, Australia
Wellington, New Zealand
Tokyo, Japan
Perth, Australia
Zurich, Switzerland
Geneva, Switzerland
Melbourne, Australia
Brisbane, Australia
Fisi wana akili kuliko Sokwe, Tafiti kadhaa zimeonesha kua Fisi wana uwezo mkubwa wa kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili (Wanajiongeza) kuliko wanyama wengine kama Sokwe.