Katika taarifa yao kwenye kikao hicho katika kaunti ya Uingereza ya Cornwall, viongozi wa G7 walisema watatoa ushirikiano "wenye misingi ya maadili, kiwango cha juu na wa uwazi."
Hatahivyo, maelezo kuhusu ni vipi mpango wa G7 utakavyofadhiliwa bado hayajawa wazi. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema kuwa kikundi hicho bado hakijafikia kwenye hatua ya kutangaza ufadhili wake kwa ajilio ya mpango huo.
Marekani hasa imekuwa mkosoaji mkubwa wa kile kinachoitwa "diplomasia ya deni" ya Uchina.
G7, ambacho ni kikundi cha viongozi wa mataifa saba yenye utajiri zaidi duniani, pia wanatarajiwa kuweka ahadi zao kwenye mpango wa kuzuia majanga yajyayo.
Hatua hizo ni pamoja na kupunguza muda unaohitajika wa kutengeneza chanjo na tiba ya Covid-19 hadi chini ya siku 100.
Waziri Mkuu wa uingereza Boris Johnson ni mwenyeji wa kikao hicho cha siku tatu kinachofanyika katika hoteli iliyopo kwenye mwambao wa bahari ya Carbis Bay katika Cornwall.
Hadi sasa ni nini ambacho nchi za magharibi zenye nguvu za mzimeifanyia uchina?
Mapema mwka huu, Marekani, Muungano wa Ulaya, Uingereza na Canada zilianzisha vikwazo vilivyoratibiwa dhidi ya Uchina.
Vikwazo hivyo vilikuwa ni pamoja na vya safari, kufuja mali, kuwalenga maafisa wa ngazi ya juu katika Xinjiang ambao wamekuwa wakishutumiwa kwa ukiukaji mkbwa wa haki za binadamu dhidi ya Waislam wa Uyghur.
Zaidi ya Wauyghur na jamii nyingine za walio wachache wanakadiriwa kuwa wamekuwa wakishikiliwa kwenye makambi yaliyoko katika jimbo la kaskazini-magharibi.
Serikali ya Uchina imekuwa ikishutumiwa kwa kuwafunga vizazi kwa nguvu wanawake wa Uyghur na kuwatenganisha watoto na familia zao.
Kwa faida hizo chache kati ya nyingi nadhani utakuwa umegundua ni kwa kiasi gani magimbi yanavyohitajika mwilini. Hivyo jitahidi kuwa mlaji wa magimbi kwa ubora wa afya yako.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.