Matumizi katika vyakula ni mengi tukihasabu asilimia 99 ya watu ulimwenguni tunatumia sana kiungo hiki ila wengi wetu hatujui kuwa mbali na hiriki kuwa kiungo katika chakula kuna faida nyingi za kiafya unaweza kupata kwa kutumia kiungo hiki.
Pia hiriki ina utajiri wa vitamins nyingi sana ambazo ni muhimu sana kata afya yetu ya mwili, vitamini vinavyopatikana katika hiriki ni kama vile vitamin A,B na C,Niacin, na Riboflavin.
Hiriki Inahimarisha afya ya mfumo wa kusaga na kusharabu chakula na pia inachochea uzalishaji wa nyongo kwa ajili ya kuyeyusha vyakula vyenye mafuta mengi mwilini hii usaidia kupunguza gas tumboni, kuondoa kiungulia na kutibu maumivu ya tumbo
Hiriki inasaidia kuleta hamu ya kula:-Kutokana uzalishaji wa nyongo kwa ajili ya kunyeyusha vyakula vya mafuta na virutubisho vingine pamoja na kuondoa gas vitu ambavyo vinachangia kuondoa hamu ya kula
Hiriki inasaidia kuimarisha mzunguko wa damu kwenye mapafu na kuzibua mirija ya hewa hivyo kuwapa unafuu wenye matatizo ya pumu, na matatizo mengine ya upumuaji