Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 29 alipata na mshtuko wa moyo na kudondoka uwanjani siku ya Jumamosi katika mchezo ambao Denmark ililala kwa bao 1-0 dhidi ya Finland huko Copenhagen on Saturday.
Daktari wa timu ya taifa ya Denmark, Morten Boesen, anasema kifaa hicho kinachojulikana kitaalamu kwa kifupi 'ICD', ni muhimu hasa wakati huu ambapo moyo wa mchezaji huyo una mipigo isio ya kawaida.
Leo timu yake ya Denmark, inarejea uwanjani kucheza na Ubelgiji, ambapo Ubelgiji imesema itasimamiosha mchezo huo katika dakika ya 10, na kutumia dakika moja kupiga makofi kama sehemu ya kukumbuka na kumtakia heri Eriksen
Mlinzi wa Uholanzi, Daley Blind aliwahi kupata tatizo la moyo mwaka 2019 lakini alirejea uwanjani February 2020 baada ya kuwekewa kifaa hicho cha ICD. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 31 yuko na timu yake hiyo ya taifa kwenye Euro 2020 , ambapo alicheza kwenye mchezo wa kufungua dimba, Uholanzi ikiizaba Ukrain 3-2.
Hata hivyo mchezaji wa zamani wa Kriketi wa England, James Taylor, 31, alilazimika kukatisha maisha yake ya kriketi, baada ya kuwekewa kifaa hicho,kufuatia matatizo ya moyo aliyoyapata mwaka 2016
Nahodha anayetimka Real Madrid Sergio Ramos, huenda akatua katika moja ya vilabu vya Paris St-Germain, Manchester City, Manchester United na Sevilla. Mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 35, aliyeanzia maisha yake ya soka Sevilla, anaondoka Real baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa miaka 16 kufutia kushindwa kuafikiana kuhusu kuongeza mkataba mpya. (AS - in Spanish)
Brighton imekataa dau la £40m kutoka Arsenal kwa ajili ya mlinzi wa England Ben White (23). Mlinzi huyo ameicheza Brighton mechi 36 za ligi kuu England msimu uliopita na kufanikiwa kuitwa timu ya taifa ya England mwezi May, mwaka huu. (Sky Sports)
Arsenal wamerudi nyuma kuhusu mpango wao wa kumsajili nyota wa kimataifa wa Norway Martin Odegaard, 22, ambapo kiungo huyo anatarajiwa kusalia klabuni kwake Real Madrid baada ya kutumia sehemu ya pili ya msimu akiwa kwa mkopo Emirates. (AS - in Spanish)
Inter Milan inajiaandaa kupambana na Everton katika mbio za kusaka saini ya mlinzi wa Uholanzi, Denzel Dumfries, 25, kutoka PSV Eindhoven. (Voetbal International - in Dutch)
Brighton imekubaliana na Stuttgart katika uhamisho ulioweka rekodi kwenye klabu hiyo wa £25m kwa ajili ya mshambuliaji muargentina Nicolas Gonzalez, 23, ambaye amepachika mabao 6 katika michezo 15 ya ligi kuu ya Ujerumami msimu wa 2020-21. (Guardian
Tottenham wanamtaka mlinzi wa kulia wa Brighton na timu ya taifa ya England chini ya miaka 21 Tariq Lamptey, 20, ambaye ameng'ara msimu uliopita akiwa na kikosi cha Graham Potter, kabla ya kupata majeraha mwezi Desemba yaliyomuweka nje ya uwanja mpaka mwisho wa msimu. (Sky Sports)
Matumaini ya mshambuliaji wa England Harry Kane, ya kutimka Tottenham kuelekea kwa mabingwa wa ligi kuu England Manchester City yanakutana na ugumu kufuatia vilabu hivyo kupangwa kucheza mechi ya kufungua pazia la ligi kuu 2021-22. (The Telegraph - subscription required)
Sheffield United huenda ikalazimika kukubali dau la Arsenal kwa ajili ya kiungo wake kutoka Norway Sander Berge. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 23 anasema anamatumaini kwamba atacheza ligi ya mabingwa Ulaya msimu ujao. (Sheffield Star)
Leeds haijakata tamaa ya kumshawishi Ezgjan Alioski,29, kuendelea kusalia Elland Road. Winga huyo wa Macedonia anatarajia kutimka kama mchezaji huru msimu huu baada ya kushindwa kuafikiana kuhusu mkataba mpya, akionekana kupunga mkono wa kwaheri katika siku ya mwisho ya msimu. (Mirror)
Crystal Palace wanatarajiwa kuzungumza na kocha wa zamani wa Borussia Dortmund Lucien Favre wakati huu wakiendelea na harakati zao za kusaka kocha mpya. (Sun)
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.