Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

"Sheria zinahitaji mgodi kukarabati mazingira na kurejesha hali ya ubora wa eneo la mgodi kuwa kama ilivyokuwa zamani. Yaani kurejesha uoto wa asili tulioukuta kabla uchimbaji wa dhahabu haujaanza. Hilo ndilo linalofanyika kwa sasa kwa kiasi kikubwa,” anasema.
 
Mawe-taka makubwa yaliyochimbwa kutoka ardhini na kurundikwa kama mlima (waste rock dump) wa mawe unaoonekana kutokea mbali na kuwa kama alama ya Buzwagi; sasa yanasawazishwa (battering) ili yasianguke, kisha yanafukiwa kwa udongo wenye rutuba na miti ya asili pamoja na ya biashara inapandwa.
 
Mbali na gharama kubwa ya kurejesha mawe-taka na udongo katika shimo hilo, Rebecca anasema kubaki kwake wazi kutatoa nafasi ya kufanyika kwa shughuli za uchimbaji katika siku za baadaye, pia kutawapa nafasi watafiti na wanafunzi wa jiolojia kujifunza aina ya miamba na miundo yake.
 
Rebecca anasema eneo pekee litakalofukiwa ni bwawa la kutunzia tope na maji yanayotoka baada ya kuchenjua dhahabu (tailings) ambayo yana mabaki ya kemikali aina ya ‘cyanide’, ambayo ni sumu; na kwamba utaalamu wa hali ya juu utatumika kutekeleza shughuli hiyo ili kuzuia madhara kwa binadamu na viumbe hai wengine.
 
Kuhusu sababu za Barrick kufunga au kusitisha uzalishaji wa dhahabu Buzwagi, Rebecca anasema: “Si kwamba dhahabu imekwisha, hapana. Ipo. Ila kwa mfumo wetu wa uendeshaji biashara, gharama ya uzalishaji kwa mitambo mikubwa kama hii tuliyo nayo inakuwa kubwa, hivyo ni hasara.
 
Wakati kazi hiyo ikiendelea, uongozi wa Barrick unajiandaa pia kukabidhi ama serikalini au kwa mamlaka zilizopo eneo hilo miundombinu mbalimbali iliyopo kama majengo, karakana, magodauni na miundombinu na mabwawa makubwa ya kuvuna maji yaliyokuwa yakitumiwa na mgodi.
 
"Huku mvua si nyingi na sisi tunatumia hadi lita milioni 10 za maji kwa siku. Kwa hiyo tumelazimika kuvuna maji ya mvua na kuyatunza. Tunaamini mabwawa haya ya kuvuna maji ya mvua yataisaidia sana Manispaa ya Kahama na kuwa chanzo kingine cha maji mbali na yale ya Ziwa Victoria, hasa kwa vijiji jirani na hapa,” anasema Rebecca, mhandisi wa mazingira aliyehitimu Chuo Kikuu cha Ardhi cha Dar es Salaam mwaka 2002 (wakati huo kikifahamika kama UCLAS).
 
Wakati mitambo mingine itahamishiwa kwenye migodi ya Barrick ya North Mara na Bulyanhulu kufuatana na taratibu za kisheria, majengo yaliyopo ndani ya Buzwagi yatabaki na yanaweza kutumiwa kama chuo, hoteli au viwanda vidogo vidogo kwa namna yoyote ambayo mamlaka husika itaona inafaa kwa wakati huo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…