Pangilia siku yako kabla ujainza; Kabla ya kuinza siku yako, andika mambo ambayo utaenda kuyafanya siku hiyo. Yapange kwa kwa kutegemea na umuhimu wake, ukianza na jambo la muhimu zaidi adi la mwisho ambalo sio muhimu sana.
Hakikisha mtu au kitu chochote akiingilii ratiba yako. Kama ni mtu hukupanga kukutana naye siku hiyo, mwambie aje siku nyingine, labda kama kuna jambo la ghafula na ni muhimu.
Kutokuwa na sababu kubwa ya kwa nini umeweka lengo.
Rafiki kuna malengo mengine tunayaweka kwa sababu tumesikia au tumeona wengine wanafanya. Kama kuna biashara tumeona inafanikiwa basi na sisi tunafungua. Kama kuna kitu tumesikia mwingine amefanya na amefanikiwa basi na sisi tunaweka lengo la kufanya.
Tunafanya kitu bila kuwa na sababu ya msingi kwa nini tunafanya. Tunafanya kitu ambacho tunajua hakiendani na dhumuni letu la maisha. Tunafanya kitu kwa sababu mtu mwingine kafanikiwa hata kama hatupendi kufanya.
Ukifanya kitu kwa sababu mwingine anafanya au umesikia kimefanikiwa ndio wewe ukafanya, inaweza kupelekee kukata tamaa hasa unapokutana na magumu au changamoto.