Watu wengi tunapoweka malengo uwa tunaweka na muda tunaotegemea kufikia malengo hayo. Lakini kuna kipindi inachukua muda mrefu zaidi ya ambavyo tulitegemea
Na hii pia imekuwa sababu kwa nini tunakata tamaa mapema, kwa sababu muda tuliotegemea kufikia lengo unakuwa umepita na bado matokeo tuliyokuwa tunategemea kupata unakuta hatujapata.
Kwanza, elewa hata kama umejiandaa kiasi gani, kuna uwezekano mkubwa usipate matokeo ndani ya kipindi ulichojiwekea. Kuna vitu vingi vitajitokeza mbele ya safari ambavyo ukutegemea.
Vipe kipaumbele vitu ambavyo vitaleta matokeo makubwa kwenye maisha yako. Usiwe mtu ambaye uko bize tu siku nzima kwa kufanya vitu ambavyo unajua havitaleta matokeo makubwa kwako.
Kwanza, elewa chochote ambacho umechagua kufanya lazima utakutana na ugumu na itakuhitaji ufanye kazi kwa bidii kabla ujapata matokeo. Kwa iyo mambo yanapokuwa magumu, ni wakati wa kuendelea kuweka juhudi na kufanya kwa nguvu zako zote.
Pili, jifunze kila siku kwa kusoma vitabu na mitandao kama huu wa Safari Ya Mafanikio na tafuta mentor au kocha wa kukasaidia na kukufundisha unapokutana na magumu.
Utafiti unaonesha ” biashara tisa (9) kati ya kumi (10) zinazoanzishwa nchini marekani uwa zinashindwa kuendela na kuishia njiani’. Mara nyingi tunaposhindwa ndio uwa unakuwa mwisho wetu. Tunashindwa kujaribu tena kwa mara nyingine na tunakata tamaa.
Rafiki naomba nikwambie kushindwa kupo. Elewa kabisa kuna kushindwa mbele ya safari unapoanza kufanya kitu kwa ajili ya malengo yako. Sisemi hivi kukutisha tamaa, Bali nakwambia ukweli.
Kushindwa ndo kunakupa kujua wapi unakosea. Kupitia kushindwa ndo unajifunza. Weka nguvu zako zote na fanya kwa bidii lakini elewa kuna kushindwa. Ukielewa hivi itakusaidia hata kama utashindwa, unaweza tena kunyanyuka na usikate tamaa.