Inaweza kuonekana kama kijikokoto kidogo chini ya ngozi, au ikikua inaweza kuonekana kama kijimpira cha gofu au hata kufikia kimpira cha tenisi kama kikiachwa bila tiba.
Kwa watoto wa kufikia hadi miaka 5, hernia hii kwa kawaida huondoka yenyewe. lakini kwa watu wazima hernia hii haipungui na huwa inazidi kuwa kubwa kila wakati.
Wanawake kwa kawaida hupata umbilical hernia wakati wa ujauzito, na hupotea yenyewe baada ya kujifungua. Kwa baadhi ya wanawake, kijishimo hiki katika musuli hubakia baada ya kujifungua. Inashauriwa kuwa wanawake wasubiri kwa miezi 3-6 kuona kama hernia hii itafunga yenyewe.
Kama ilivyo kwa hernia nyingine, dalili za kawaida ni maumivu kwenye kitovu. Kutokana na mafuta au misuli kupita kwenye hernia hii, uvimbe utaonekana chini ya ngozi kwenye eneo hilo.
Baada ya muda, kama hernia itakuwa kubwa sana, utumbo unaweza kunaswa kwenye hernia hiyo na kuleta madhara kwenye utumbo, vikiambatana na kichefuchefu, kutapika, na kufunga choo.
Sababu Za Hernia
Ukiondoa hernia inayotokana na upasuaji wa awali, mara nyingi hakuna sababu inayoeleweka ya kusababisha hernia. Watu walio kwenye hatari zaidi ya kupata hernia ni wenye umri mkubwa, na wanaume wapo kwenye hatari zaidi kuliko wanawake.
Kikozi cha mara kwa mara
. Kuwa na tatizo la cystic fibrosis
. Kuvimba kwa tezi dume
. Unene wa kupindukia
. Kukojoa kwa shida
. Kunyanyua vitu vizito
. Maji tumboni
. Lishe duni
. uvutaji wa tumbaku
. Korodani zisizoshuka
. Uchovu wa mwili
Lakini wakati mwingine, inaweza kukukosesha raha na kuwa na maumivu, dalili zikiongezeka wakati umesimama au wakati unanyanyua vitu vizito. Watu wengi huona uvimbe ukizidi na hatimaye humwona daktari.
Kuna wakati ambapo hernia inahitaji huduma ya haraka ya upasuaji, kwa mfano, pale sehemu ya utumbo inapokuwa imezibwa na hernia ya tumbo (inguinal hernia).
Dunia na sayari zingine havizunguki Jua bali vinazunguka katikati ya mfumo wa Jua sehemu ambayo ipo nje ya Jua. Sehemu inayozungukwa na sayari inaitwa Barycenter.