Shimo hili linajulikana kama Crater of Darvaza ,lililopo kaskazini mwa lliliokuwa taifa la Muungano wa Usovieti la Turkmenistan.
''Wakati nilipoliona shimo hilo kwa mara ya kwanza na kulikaribia huku upepo wenye joto kali uliokuwa ukitoka ndani yake ukinipiga usoni , nilihisi kwamba hili ni eneo ambalo shetani anaweza kujitokeza ndani yake'' , alisema mtafiti wa Canada George Kourounis akizungumza na BBC.
Likiwa na upana wa mita 69 na kina cha mita 30 , shimo hilo limekuwa likitoa gesi asilia ambayo imekuwa ikichomeka kwa miongo kadhaa sasa