Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Wakati kukiwa na zaidi ya aina 30 tofauti za aina ya mtama, aina moja tu ndio huvunwa kwa matumizi ya binadamu, wakati aina nyingine zilizobaki hutumika kama malisho kwa wanyama.
 
Ikiongezwa kwenye diet, inaweza kutoa vitamin kama niacin, riboflavin, na thiamin, vilevile pia kiwango kikubwa cha magnesium, iron (madini joto), shaba (copper), calcium, phosphorus, na potassium, na karibia nusu ya protini inayohitajika kwa siku na nyuzi lishe (dietary fiber) muhimu zinazotakiwa.
 
HUBORESHA AFYA YA UMENG'ENYAJI CHAKULA
Mtama ni moja ya chakula bora zaidi kwa dietary fiber. Kikombe kimoja kilichojaa punje za mtama kina gramu 12.9 za dietary fiber, ikiwa na maana kwamba njia yako ya umeng'enyaji itafanya chakula chako kupita bila shida, kuzuia kufungamana njiani, kutopata choo, maumivu ya tumbo, gesi kuzidi, na kuharisha.
 
Zaidi, kiasi cha nyuzi lishe (dietary fiber) kinachozidi kwenye mwili husaidia kukwangua na kuondoa cholesterol hatari (LDL), ambayo huboreaha afya ya moyo na kuulinda mwili wako na dalili za atherosclerosis, mshutuko wa moyo, na kiharusi.
 
INAWEZA KUSAIDIA KUZUIA KANSA

Utafiti uliofanyika 2018 na watafiti wa kimarekani ulipendekeza kwamba mtama wenye utajiri wa polyphenol unaweza kuwa na kizuia-kansa na ushaihidi wa kisayansi unahitajika. Utafiti mwingine ulichapishwa kwenye jarida la 'PLoS One' unaelezea kwamba mtama unatabia ya kiashiria cha kuzuia ukuaji wa kansa na kizuia uvimbe (anti-tumor) na inaweza kuzuia kansa muendelezo wa kansa kama vile kansa ya titi. Pia vilevile ina athari za kuzuia shida ya njia ya chakula.
 
Hudhibiti Ugonjwa wa Kansa
Utumiaji uliokithiri wa carbohydrate huvunjwavunjwa kwenda kuwa sukari nyepesi na kusababisha uharibifu makubwa kwenye kiwango cha glucose kwenye mwili, kupelekea mtu kupata Kisukari, au kusababisha mtafaruku kwa watu wenye ugonjwa wa kisukari tayari.
 
Hatahivyo, ganda la nje lenye utajiri wa tannin lina enzymes zinazozuia mwili kuingiza starch, amabyo inaweza kusaidia kudhibiti kiwango cha insulin na glucose kwenye mwili. Kwa maana hiyo basi, wenye ugonjwa wa kisukari hawatapata shida za hapa na pale katika kiwango cha glucose yao.
 
Kwa bahati nzuri, jarida la 'Clinical Nutrition' lilichapisha utafiti uliofanywa kwa pamoja, ambapo liliangazia kwamba nafaka mbadala kama mtama, zinaweza kuliwa kwa usalama na wale wanaosumbuliwa na tatizo hilo linalozidi kuongezeka, bila maumivu ya uvimbe, kichefuchefu, na uharibifu wa utumbo unaosababishwa na gluten.
 
Huimarisha Afya ya Mifupa
Magnesium ipo katika viwango vya juu sana kwenye mtama, ina maanisha kiwango chako cha Calcium kitakuwa kimedhibitiwa, kwani magnesium huongeza uingizwaji wa calcium kwenye mwili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…