Barcelona itamuwania kiungo wa kireno wa Wolves Ruben Neves, 25, kama mbadala wa nyota wake wa kimataifa wa Hispania Sergio Busquets, 33. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Mlinzi wa zamani wa Manchester United Rio Ferdinand anaamini klabu hiyo ya Old Trafford inapaswa kujaribu kumsajili mlinzi wa kati wa Paris St-German Mbrazil Marquinhos, 27, na nyota wa kimataifa wa Uruguay anayekipiga BarceloRonald Araujo, 23, ili kuimarisha safu yake ya ulinzi. (MEN)
Wadau nimeona mada nyingi zilianzishwa kwenye jukwaa hili zikihusisha google adsense ila wadau walioanzisha mada hizo hawakuongelea kwa upana kuhusu google adsense pamoja na dependencies zake: kwenye uzi huu naomba mdau kama una shauku ya kuijua vizuri google adsense basi kaa mkao wa kula...
Hata hivyo, rais wa Barcelona Joan Laporta amekanusha madai kwamba mashauriano ya kumsajili Haaland ambaye pia anatakiwa na Manchester City na Real Madrid tayari yanaendelea. (Mail)
Newcastle United wanataka kumsajili mlinzi wa Ujerumani Antonio Rudiger wakati mkataba wa kiungo huyo wa Chelsea wa miaka 29-utakapomalizika mwisho wa msimu huu. (Telegraph)
Arsenal huenda wakajaribu kumsajili tena winga wa Ujerumani Serge Gnabry kutoka Bayern Munich, huku thamani ya kiungo huyo wa miaka 26 - aliyekuwa na Gunners kwa miaka minne - ikikadiriwa kuwa £63m. (Football.London)
Mshambuliaji wa Uingereza Harry Kane, 28, amewaambia wachezaji wenzake kwamba atasalia Tottenham msimu ujao ikiwa watafuzu kwa soka ya Ligi ya Mabingwa na Antonio Conte atabaki kama kocha. (Express)
Tottenham wanajiandaa kupokea maombi ya kumununua mlinzi wa miaka 23- Mbrazil Emerson Royal, chini ya mwaka mmoja baada ya kumnunua kwa £26m kutoka Barcelona. (Sun)
Liverpool watapata fursa ya kumsajilimshambuliaji wa Red Bull Salzburg wa miaka 20- Mjerumani Karim Adeyemi msimu wa joto dirisha la uhamisho litakapofunguliwa, hata hivyo, huenda wakakabiliwa na ushindani kutoka kwa Borussia Dortmund. (Express)
Manchester United watalazimika kulipa hadi euro milioni 80 (£66m) kumsajili kiungo wa kati wa Serbia Sergej Milinkovic-Savic, 27, kutokana Lazio kuchukua nafasi ya kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 28. (Sport Witness)
Winga wa zamani wa Arsenal Perry Groves anasema Gunners wanatakiwa kumlenga mshambulizi wa Everton na Uingereza Dominic Calvert-Lewin, 24, mwisho wa msimu. (Star)
Juventus wamewasiliana na wakala wa Paul Pogba Mino Raiola kuhusu uwezekano wa kiungo huyo wa kati wa Manchester United kurejea Turin msimu ujao. (Gazzetta dello Sport - in Italian)
Pogba itabidi akubali kupunguziwa mshahara iwapo atarejea Juve, ambao wanaona harakati zao za kumpata itakuwa ngumu huku Paris St-Germain na Real Madrid zikiwamo pia katika kinyang'anyiro cha kumnasa Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 28. (Calciomercato - kwa Kiitaliano)
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.