Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Real Madrid wanamlenga kiungo wa kati wa Borussia Dortmund na Uingereza Jude Bellingham, licha ya mchezaji huyo wa miaka18 kuhusushwa na uhamisho wa Liverpool. (Bild)
 
Mlinzi wa Manchester United wa miaka 21- Muingereza Brandon Williams - ambaye kwa sasa yuko Norwich kwa mkopo -anasema "hakuna haja" ya yeye kurudi Old Trafford kama mchezaji wa ziada. (Mail)
 
Barcelona wanamatumaini ya kumsajili kwa mkopo winga wa Uhispania Adama Traore, 26, kutoka Wolve. (RAC 1 - via Goal)
 
Atletico Madrid huenda wakarefusha mkataba wa mkopo wa mshambuliaji Antoine Griezmann,31, kutoka Barcelona lakini hawako tayari kumuachilia mshambuliaji wa Portugal Joao Felix, 22, ajiunge na miamba hao wa Uhispania. (Goal)
 
Arsenal wako tayari kumuachilia kiungo wa kati wa Uruguay wa miaka 26- Lucas Torreira - ambaye kwa sasa anachezea currently Fiorentina kwa mkopo - kuondoka kabisa msimu huu wa joto, huku kungo wa kati wa miaka 29- Mmisri Mohamed Elneny pia akijiandaa kuondoka. (Fabrizio Romano)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…