Leicester City ina matumaini ya kumshawishi kiungo wa Ubelgiji Youri Tielemans, 24, kusaini mkataba mpya, licha ya kusakwa na vilabu vya Manchester United Arsenal. (Team Talk)
Kiungo Mbrazil Douglas Luiz, 23, anaweza kuondoka Aston Villa msimu huu, huku Meneja wa timu hiyo Steven Gerrard akiipa kipaumbele kikubwa nafasi ya kiungo mkabaji kwenye usajili wa msimu ujao. (Mail)
Beki ya kupanda ya Middlesbrough Djed Spence, anayecheza kwa mkopo Nottingham Forest, anataka kuhamia ligi kuu- huku Arsenal na Tottenham zikuhusishwa na uhamisho wake wa gharama ya £20m mwishoni mwa msimu. Manchester United pia inamtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa England chini ya miaka-21. (Mirror)
Nottingham Forest inataka kubadili mkopo wa kiungo muingereza James Garner, 21 kutoka Manchester United kuwa usajili wa kudumu mwishoni mwa msimu, lakini hilo litategemea kama watafanikiwa kupanda daraja kucheza ligi kuu England. (Football Transfers)
RB Leipzig wanajiandaa kufanya mazungumzo ya mkataba mpya na kiungo mfaransa Christopher Nkunku, 24, msimu huu, lakini watasikilia madau yakayovuka au kufikia £63.3m.
Manchester United, Liverpool, Paris St-Germain, Real Madrid, Manchester City, Arsenal na Bayern Munich zote zinafuatilia hali ya mambo kwa karibu. (ESPN)
Manchester United wako tayari kumnunua mshambuliaji wa Uingereza Tammy Abraham, 24, ambaye amefunga mabao 23 katika klabu ya Roma ya Italia msimu huu. (Corriere dello Sport -In Italian)
Mshambuliaji wa Ufaransa Anthony Martial, 26, anaweza kutumiwa na Manchester United kama suluhu katika mpango wa kumsaini nahodha wa Uingereza Harry Kane, 28, kutoka Tottenham. (ESPN)
Kiungo wa kati wa Uingereza Kalvin Phillips, 26, ameiambia Leeds United kuwa anataka kusaini mkataba mpya msimu huu, ambao unaweza kuwakatisha tamaa Manchester United, Liverpool, Newcastle, West Ham na Aston Villa . (Mirror)
Everton italazimika kumuuza mmoja wa washambuliaji wake nyota, mshambuliaji wa Uingereza Dominic Calvert-Lewin, 25, au mchezaji wa kimataifa wa Brazil Richarlison, 24, msimu wa joto baada ya kupata hasara ya £121m msimu uliopita.(Sun)