Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Spurs wanaweza kutumia kipengele cha kumsajili Kulusevski kwa mkataba wa kudumu kwa pauni milioni 25, badala ya kusubiri hadi mkopo wake umalizike, wakati chaguo hilo linaweza kugharimu pauni milioni 33.5. (Times - subscription required)
 
Mlinzi wa Manchester United wa miaka 21- Muingereza Brandon Williams - ambaye kwa sasa yuko Norwich kwa mkopo -anasema "hakuna haja" ya yeye kurudi Old Trafford kama mchezaji wa ziada. (Mail)
 
Barcelona hawajawasilisha ofa ya kumnunua mshambuliaji wa Leeds Raphinha, lakini makubaliano ya kibinafsI yamejadiliwa na wakala wa nyota huyo wa miaka 25. Winga huyo raia wa Brazilia ana kifungu katika mkataba kinachoamua bei yake ikiwa klabu yake itashushwa daraja. (Fabrizio Romano)
 
Atletico Madrid huenda wakarefusha mkataba wa mkopo wa mshambuliaji Antoine Griezmann,31, kutoka Barcelona lakini hawako tayari kumuachilia mshambuliaji wa Portugal Joao Felix, 22, ajiunge na miamba hao wa Uhispania. (Goal)
 
Arsenal wako tayari kumuachilia kiungo wa kati wa Uruguay wa miaka 26- Lucas Torreira - ambaye kwa sasa anachezea currently Fiorentina kwa mkopo - kuondoka kabisa msimu huu wa joto, huku kungo wa kati wa miaka 29- Mmisri Mohamed Elneny pia akijiandaa kuondoka. (Fabrizio Romano)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…