Lakini Newcastle wanatazamiwa kukosa lengo moja kwani AC Milan wamekubaliana na mlinzi wa kati wa Lille Mholanzi Sven Botman mwenye umri wa miaka 22 kufuatia mazungumzo ya wiki iliyopita. . (90min)
The Magpies wameweka orodha ya wachezaji saba wanaotamani kuhama ambayo pia inajumuisha mshambuliaji wa Everton na Uingereza Dominic Calvert-Lewin, 25. (Mirror)
Licha ya kutakiwa na Manchester United na Liverpool, mlinzi wa Uruguay Ronald Araujo, 23, anakaribia kuafikiana mkataba mpya wa muda mrefu na Barcelona, wakala wake amethibitisha. (ESPN)
Tottenham wanatarajiwa kuanzisha chaguo lao la kumsajili winga wa Uswidi Dejan Kulusevski, 21, kutoka Juventus katika nafasi ya kwanza msimu huu wa joto. (Mail)
Spurs wanaweza kutumia kipengele cha kumsajili Kulusevski kwa mkataba wa kudumu kwa pauni milioni 25, badala ya kusubiri hadi mkopo wake umalizike, wakati chaguo hilo linaweza kugharimu pauni milioni 33.5. (Times - subscription required)
Kwa wale waliopita jeshini na wanatamani kupata ajira za kijeshi na siyo za Knight Support basi Urusi imetangaza ajira kibao. Watakaopigana mstari wa mbele malipo ni $7000 na unapewa $50,000 za kuachia familia unapoondoka. Watakaopigana mstari wa nyuma kama wasaidizi wa wapiganaji malipo ni...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.