Likishakuwa gumu ni vigumu kufinyanga tena mpaka uvunje/ukisage chombo hicho cha udongo na ukichanganye na maji kilainike tena na ndio utengeneze umbo lingine ambalo unalitaka.
Kama vile ilivyochukua muda kuzoea mwili na akili kuzoea mazoea mabaya ndivyo itakavyochukua muda mwili na akili kujenga mazoea mapya tunayoyataka katika maisha yetu.
Mawazo yako hupelekea matendo, matendo hupelekea mazoea, mazoea hupelekea kujenga sifa yako na sifa yako hujenga hali uliyonayo ya maisha yako kwa sasa.