Liverpool inamtaka winga wa Villarreal na Uholanzi Arnaut Danjuma, 25, kuchukua nafasi ya mshambuliaji Sadio Mane, lakini Liverpool haina mpango huo kwa sasa hadi mwaka 2023. (Goal)
Kama kocha wa Ajax Erik ten Hag akichaguliwa kuwa meneja wa Manchester United kama invyotarajiwa, basi atamsajili kiungo wa kati wa Portugal Ruben Neves, 25, Kutoka Wolves. (Sun)
Wakala wa mchezaji wa Chelsea na Ujerumani Timo Werner, 26, yupo nchini Italia akikutana na AC Milan, Juventus na Atalanta . (Corriere dello Sport - in Italian)
Paul Pogba , 29, anapendelea kurudi Juventus kuliko kwenda Paris St-Germain baada ya muda wake kuisha majira ya joto. Lakini kwa upande wa Italia wana wasiwasi kuhusu pesa anazotaka kulinganisha na umri wake (Tuttosport - in Italian)
Winga wa PSV Eindhoven na Uholanzi Cody Gakpo, 22, ameweka wazi mapenzi yake kwa Arsenal huku akiendelea kuunganishwa na wenyeji wa vilabu vingine ikiwemo Manchester United na Liverpool. (Goal)
Barcelona ina Imani kuwa ina nafasi kubwa ya kumsajili mshambuliaji wa Bayern Munich na Poland Robert Lewandowski, 33, msimu huu wa majira ya joto. (Sport - in Spanish)
Mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 23, anaweza kutia Saini mkataba mpya katika klabu yake ya Paris St-Germain mbali na kuonesha nia kwa Real Madrid. (Sky Sports)
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.