Hii ni dalili ya upungufu wa vitamin K ambayo husaidia kugadisha damu hasa wakati ukiwa umeumia. Kula spinach kwa wingi kutasaidia hali hii kupungua au kuacha kabisa.
Spinanchi ina kiasi kingi cha madini ambayo yana faida nyingi mwilini. Madini hayo ni pamoja na potasiam, chuma, manganizi, zinki na copper. Madini haya husaidia kuimarisha mifupa na meno ya mtumiaji.
Virutubisho vilivyo katika spinachi kusagwa kwa urahisi na kubadilika kuwa amino acid ambayo ni muhimu kwa mwili wa binadamu. Acid hii huimarisha mishipa na husaidia kuponya vidonda kwa haraka
Protini inayopatikana katika mboga hii husaidia mmeng’enyo wa chakula kufanyika kwa urahisi na hivyo husaidia kupata haja kubwa kwa urahisi na husaidia kutibu kukosa choo.
Kansa ni moja ya mgonjwa mabaya sana ambayo yanatesa watu wengi. Inasemekana kuwa ulaji wa Spinachi kwa wingi husaidia kuzuia na hata kutibu ugonjwa huu.
Spinachi ni moja ya mboga ya majani zenye virutubisho vingi sana na ina faida nyingi katika mwili wa binadamu. Kama utaweza kuiongeza katika milo yako kila siku, itakusaidia sana kuimarisha afya yako kwa kiasi kikubwa
Ulaji wa vyakula vyenye virutubisho vinavyohitajika mwilini kuna kuhakikishia afya bora na hii itakusaidia sana kupunguza kuingiza kemikali nyingi mwilini unapokuwa unaumwa kwa kutumia dawa.
Kinga ni bora kuliko tiba! Kula vyakula ambavyo vinaimarisha afya yako na si vinavyodumaza afya yako kama vyakula vyenye mafuta mengi na vyakula vilivyokoborewa.
Mboga hii inaweza kuliwa kwa chakula chochote; iwe ugali, wali, inaweza pia kutumika kungenezea juisi nzito (smoothie) Ni nzuri pia kutengezea kachumbari, supu ya mbogamboga. Uamuzi ni wako tu ni kitu gani unapenda
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.