Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Huimarisha afya ya mifupa

Spinanchi ina kiasi kingi cha madini ambayo yana faida nyingi mwilini. Madini hayo ni pamoja na potasiam, chuma, manganizi, zinki na copper. Madini haya husaidia kuimarisha mifupa na meno ya mtumiaji.
 
Virutubisho vilivyo katika spinachi kusagwa kwa urahisi na kubadilika kuwa amino acid ambayo ni muhimu kwa mwili wa binadamu. Acid hii huimarisha mishipa na husaidia kuponya vidonda kwa haraka
 
Protini inayopatikana katika mboga hii husaidia mmeng’enyo wa chakula kufanyika kwa urahisi na hivyo husaidia kupata haja kubwa kwa urahisi na husaidia kutibu kukosa choo.
 
Inasaidia kutibu na kuzuia kansa

Kansa ni moja ya mgonjwa mabaya sana ambayo yanatesa watu wengi. Inasemekana kuwa ulaji wa Spinachi kwa wingi husaidia kuzuia na hata kutibu ugonjwa huu.
 
Spinachi ni moja ya mboga ya majani zenye virutubisho vingi sana na ina faida nyingi katika mwili wa binadamu. Kama utaweza kuiongeza katika milo yako kila siku, itakusaidia sana kuimarisha afya yako kwa kiasi kikubwa
 
Ulaji wa vyakula vyenye virutubisho vinavyohitajika mwilini kuna kuhakikishia afya bora na hii itakusaidia sana kupunguza kuingiza kemikali nyingi mwilini unapokuwa unaumwa kwa kutumia dawa.
 
Mboga hii inaweza kuliwa kwa chakula chochote; iwe ugali, wali, inaweza pia kutumika kungenezea juisi nzito (smoothie) Ni nzuri pia kutengezea kachumbari, supu ya mbogamboga. Uamuzi ni wako tu ni kitu gani unapenda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…