Naamini unapenda kupata maarifa kwa kuufahamu mwili wako vyema. Karibu ufuatilie makala hii ili nikujuze mambo 25 yakukushangaza kuhusu mwili wa binadamu.
Uwezo mkubwa wa kufikiri unahusiana na kiasi cha ndoto mtu anazoota
Inaaminika kuwa watu wenye uwezo mkubwa wa kufikiri (Intelligent Quotient – IQ) huota ndoto nyingi zaidi kuliko watu wenye IQ ndogo. Hili kwako likoje? Naamini utatupa maoni yako hapo chini.
Kwikwi ni mkazo wa ghafla na usio wa hiari wa misuli ya kiwambo unaosababisha pumzi kutokea kinywani na sauti ya kugugumia kutokana na hewa kuingia kwenye umio. Hivyo tafiti zimebaini kuwa wanaume hupata kwikwi mara mbili zaidi ya wanawake.
Utafiti umebainisha kuwa uwezo wa kusikia hupungua pale mtu anapokuwa ameshiba sana. Labda hii ndiyo sababu watu wengi hawawi wasikivu baada ya kula sana; hasa wanafunzi shuleni.
Mtoto mchanga hutambua rangi nyeusi na nyeupe pekee
Inaelezwa kuwa mtoto mchanga hatambui rangi nyingine zaidi ya nyeusi na nyeupe pekee. Hii ni kusema kuwa ulimwengu wote kwa mtoto ni mweusi na mweupe pekee.
Konea (cornea) sehemu angavu ya mbele kwenye jicho. Hii ni sehemu pekee kwenye mwili isiyokuwa na damu; sehemu hii hupata oksijeni moja kwa moja kutoka kwenye hewa.
Asilimia 75 ya ubongo ni maji
Naamini unafahamu kuwa asilimia 70 ya mwili wa binadamu ni maji. Lakini je wajua kuwa asilimia zaidi ya 75 za ubongo wa binadamu ni maji? Fahamu hili sasa.
Nywele zinaweza kuishi kwa miaka 3 hadi 7
Je wajua kuwa nywele za binadamu ni sehemu hai ya mwili? Nywele za binadamu zinaweza kuishi kwa miaka 3 hadi 7.
Meno huanza hukua miezi 6 kabla ya kuzaliwa
Ingawa mtoto mchanga napozaliwa meno yake yanakuwa bado hayajachomoza kwa nje, lakini yanakuwa tayari yameshaanza kuota kwa ndani miezi sita kabla ya kuzaliwa.
Figo yako ina vichujio milioni moja
Kila figo yako moja ina vichujio takriban milioni moja vinavyochuja lita 1.3 za damu kila dakika na kupelekea kuzalisha lita 1.5 za mkojo kwa siku.
Binadamu wengi hawawezi kuchezesha masikio yao
Inasemekana ni watu wachache pekee ndiyo wanaoweza kuchezesha masikio yao duniani. Je wewe unaweza? Ikiwa unaweza basi uko kati ya hao wachache.
Pua ya binadamu inaweza kubaini harufu trilioni moja
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Leslie Vosshall kwenye chuo cha Rockefeller, ulibaini kuwa pua ya binadamu inaweza kubaini harufu tofauti takriban trilioni moja. Kiwango hiki ni tofauti na kilichokuwa kinafahamika mwanzo cha harufu 10,000.
Ndevu za mwanaume zinaweza kufikia mita tisa
Inaelezwa kuwa ikiwa mwanaume hatonyoa ndevu katika maisha yake yote; ndevu zake zinaweza kukua na kufikia urefu wa mita tisa.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.