Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Historia ya jina Kariakoo na Soko la Kariakoo inaanzia enzi za Ukoloni wa Mjerumani wakati Tanzania Bara ikiitwa Tanganyika.

Mahala lilipo Soko la Kariakoo palijengwa jengo la utawala wa Wajerumani ambalo lilikusudiwa litumike kama ukumbi wa kuadhimishwa na kutawazwa kwa Mfalme Kaiser Wilheim wa Ujerumani kwa wakati huo.

Lakini mara tu baada ya jengo kukamilika, Vita kuu ya Kwanza ya Dunia ilianza na Waingereza walipouteka mji wa Dar es Salaam, walilitumia jengo hilo kama kambi ya jeshi kwa askari waliojulikana kama “Carrier Corps” kwa jina la kigeni, yaani wabeba mizigo likitafsiriwa kwa Kiswahili.

Jina hilo la maaskari wabeba mizigo katika Kiswahili lilitamkwa “karia-koo” na liliendelea kutumika kama jina la eneo lote linalozunguka eneo lilipo jengo hilo la soko la Kariakoo.

Baada ya vita Kuu ya Kwanza ya Dunia kuisha mwaka 1919 na nchi kuanza kutawaliwa na Waingereza , jengo hilo lilianza kutumika kama Soko na kuhudumia wakazi wa mji huu.

Wakati huo wafanyabiashara walikuwa wakiuza bidhaa zao sakafuni kwa sababu hapakuwa na meza. Wafanyabiashara waliendelea kufanya biashara sakafuni hadi miaka ya 1960 wakati meza za saruji zilipojengwa.

Kwa kadri Jiji la Dar es Salaam lilivyokua na wakazi wake kuongezeka, ndivyo Soko hilo la zamani lilivyokuwa likishindwa kumudu kutoa huduma nzuri kwa wananchi.

Pamoja na kubanana katika soko hilo na biashara kufanyika katika mazingira yasiyoridhisha, pia halikuwa na ghala za kuhifadhia bidhaa. Hali hiyo iliwafanya viongozi wa Halimashauri ya Jiji kuona haja ya kuwa na soko kubwa na la kisasa kulingana na maendeleo ya Jiji na hivyo wakaanza kujadili uwezekano wa kujenga soko jipya.

Uamuzi wa kujenga Soko Kuu la Kariakoo la sasa, ulifanywa na Serikali mnamo mwaka 1970.

Serikali iliagiza Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kujenga Soko jipya la kisasa ambalo lingechukua nafasi ya Soko la zamani.

Mipango yote ilikamilika na ujenzi ulianza rasimi mwezi Machi 1971.

Ramani ya jengo la Soko ilitayarishwa na mchoraji wa ramani za majengo Injinia Mtanzania Beda J. Amuli

Shughuli za ujenzi zilikamilika mwezi Novemba 1975, na lilifunguliwa rasmi 08/12/1975 na Rais Nyerere
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…