Mnyama anayefahamika kwa jina la kigeni Capybara ambapo kwa kiswahili huitwa Ngekewa ni mnyama mwenye ukubwa wa sentimita 134 na uzito unaokadiliwa kuwa kilo 66 anapokuwa mkubwa na mnyama huyu asili yake ni nchi ya America ya kusini.
Huyu Ngekewa ndio mnyama anayependwa na viumbe vingi vya porini na majumbani.
Wanyama kama mamba, chatu, nyani, paka, kobe na hata ndege wa aina mbali mbali hupenda kukaa karibu naye na kufurahia maisha hivyo mnyama huyu huhesabika kama kiumbe chenye bahati ya kupendwa na viumbe wengine ukiondoa maadui zake.
Kwenye kamusi ya lugha ya kiswahili neno Ngekewa mbali na kumzungumza huyu mnyama pia limetafsiliwa kama bahati au yenye bahati na ndio maana hata mtaani mtu mwenye bahati huambiwa ana ngekewa.
𝗠𝗮𝗯𝗮𝗱𝗶𝗹𝗶𝗸𝗼 𝗮𝗺𝗯𝗮𝘆𝗼 𝘆𝗮𝗻𝗮𝗮𝗻𝘇𝗮 𝗸𝘂𝘄𝗲𝗸𝘄𝗮 𝗻𝗶: 1️⃣ 𝗥𝗲𝗮𝗰𝘁𝗶𝗼𝗻𝘀 - ni mfumo wa kuchagua emoji kuonyesha mwitikio wako katika message. Ni kama iMessage, Instagram DM na Facebook
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.