Tottenham watakuwa kwenye soko la kutafuta beki wa kati wa upande wa kushoto msimu huu wa joto na wanafuatilia hali ya mlinzi wa Uhispania Mario Hermoso, 26, huko Atletico Madrid. (Mail)
Borussia Dortmund wameafikia makubaliano ya kimsingi na Red Bull Salzburg kuhusu kumsajili Karim Adeyemi lakini fowadi huyo wa Ujerumani, 20, bado yuko kwenye mazungumzo na Liverpool, RB Leipzig na Paris St-Germain. (Sky Sport Germany - in German)
Manchester United walikuwa na skauti kwenye ushindi wa RB Leipzig wa Ligi ya Europa Alhamisi kumtazama mshambuliaji wa Ufaransa Christopher Nkunku, 24, ambaye alifunga mabao mengine mawili na kufikisha 30 msimu huu. (Nicolo Schira, Twitter)
Tottenham wana uhakika wa kupata ofa ya kumnunua mlinda mlango wa West Bromwich Albion anayecheza na timu ya taifa ya Uingereza Sam Johnstone, 29, licha ya kutakiwa na Manchester United(Express)
Barcelona wameongeza kasi katika kumsaka nahodha wa Chelsea Cesar Azpilicueta, 32, huku beki huyo wa Uhispania akishinikiza kuondoka huku kukiwa na hali ya sintofahamu ya kifedha huko Stamford Bridge. (Sport - in Spanish)
Paolo Dybala, 28, anapanga kufanya mazungumzo na Arsenal na Tottenham huku kandarasi ya mshambuliaji huyo wa Argentina katika klabu ya Juventus ikitarajiwa kumalizika msimu wa joto. (Express, via Corriere Dello Sport)
Vilabu vingi vya Ulaya na Premier League vinajipanga kumpiga bei beki wa kati wa Torino raia wa Brazil Gleison Bremer, huku Arsenal, Leicester, Everton na Newcastle wakiwa wamewasiliana na klabu hiyo ya Serie A.
Tottenham na Atletico Madrid wametuma maskauti huko Turin, na Bayern Munich na Borussia Dortmund pia wanamfuatilia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. . (Gazzetta Dello Sport - in Italian)
Kiungo wa kati wa Ubelgiji Eden Hazard, 31, hataki kuondoka Real Madrid msimu huu wa joto, licha ya Arsenal, AC Milan na Borussia Dortmund kutajwa kuwa wanunuzi. (RTBF, via RTL Sport - in French)
Manchester City bado wanamfuatilia Erling Braut Haaland, 21, lakini wangependelea kuepuka kuamsha kipengele cha kutolewa cha mshambuliaji huyo wa Norway cha pauni milioni 63, ambacho watalazimika kulipa kwa mkupuo mmoja.
Beki wa The Gunners wa Brazil Gabriel Magalhaes, 24, anasema anafuraha na ameangazia taaluma yake huko Emirates, huku kukiwa na tetesi za kutakiwa na Barcelona. (Fabrizio Romano)
Fenerbahce na Galatasaray wanataka kumsajili James Rodriguez wa Al Rayyan msimu huu wa joto lakini winga huyo wa Colombia, 30, ana nia ya kujiunga na Atletico Madrid. (FotoMac, via Mundo Deportivo - in Spanish)
Mshambuliaji wa Liverpool Mmisri Mohamed Salah anasema sio muda unafaa kuzungumzia kuhusu mazungumzo ya mkataba wake yanayoendelea na klabu yake, ambayo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 ameyaeleza kama "hali ya siri". (Sky Sports)
Barcelona ainamini winga Mfaransa mwenye umri wa miaka 24, Ousmane Dembele, ambaye atakuwa huru katika msimu wa kiangazi, atajiunga na Paris St-Germain kama mshambuliaji Kylian Mbappe, 23, ataondoka katika klabu hiyo ya Ufaransa. (El Nacional - in Catalan)
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.