Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mtu angeweza kufungwa kwenye nguzo na kuchomwa moto; wangeweza kutupwa kwenye uwanja (wa sarakasi) kupigana na wanyama pori hadi kufa; au mtu angeweza kusulubishwa, kama ilivyotokea kwa Yesu", anaeleza mwanahistoria André Leonardo Chevitarese, mwandishi wa 'Yesu wa Nazareti: Hadithi Nyingine' na profesa wa programu ya wahitimu katika Historia Linganishi katika Taasisi ya Historia ya Chuo Kikuu cha Shirikisho cha Rio de Janeiro (UFRJ )
 
Ingawa hakukuwa na kesi ya kweli, sababu za kilimwengu zilizosababisha kifo cha mwanadamu Yesu zinajulikana. Na sababu zilikuwa za kisiasa. Ndio, Yesu alikuwa mfungwa wa kisiasa, aliyehukumiwa kifo kwa, kwa maoni ya wenye mamlaka, shambulio dhidi ya utaratibu ulioanzishwa na mamlaka ya Kirumi.
 
Kimsingi, alishutumiwa kuwa mlaghai. Mashtaka haya yalitoka kwa viongozi wa kidini wa Wayahudi walioishi hapo wakati huo na ambao walimtambulisha kama adui wa Kaisari, kama mtu aliyejionesha kuwa 'mfalme'", anahoji. Mwana Vatican. Filipe Domingues, naibu mkurugenzi wa taasisi ya Kikatoliki ya The Lay Centre huko Roma.
 
Mazingira hayo yalikuwa na msukosuko kwa muda mrefu, kukiwa na migogoro ya kisiasa na ukandamizaji wa watawala," anasema mwanahistoria, mwanafalsafa na mwanatheolojia Gerson Leite de Moraes, profesa katika Chuo Kikuu cha Presbyterian cha Mackenzie.
 
Kwa mantiki hiyo, hii inawaelemea sana watu maskini zaidi, kwa sababu kuna watu waliotawaliwa zaidi na kuna baadhi ya wasomi wanafanya makubaliano na watawala, ikiwa ni pamoja na mikataba ya kisiasa, na wakati mwingine ushirikiano wa kiuchumi unaoridhisha," anaongeza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…