Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kwa hiyo, kulingana na simulizi hii, Pilato angenawa mikono yake kuonesha kwamba hakuwa na sababu ya kuuliwa.

Katika sura ya 23 ya Injili ya Luka, andiko hilo linasema kwamba "wakaanza kumshitaki, wakisema: Tumemwona mtu huyu akilipotosha taifa, akikataza kutolipa kodi kwa Kaisari, na kusema kwamba yeye mwenyewe ndiye Kristo Mfalme.
 
Kilichokuwa muhimu kwa Roma ilikuwa maudhui ya kisiasa. Kwa maneno mengine: ikiwa mtu alikataa kulipa kodi, mtu huyo angeweza kuwatia moyo watu wengine na kuwaongoza kuasi dhidi ya kulipa kodi. Hili linaweza kuishia kuwa tatizo kwa Roma" anachambua mwanahistoria.
 
Katika muktadha huu, ni muhimu kukumbuka kwamba Roma iliishi katika kipindi kinachojulikana kama Pax Romana.

Kipindi hiki cha utawala wa maeneo mengine, chenye dhamana za usalama na ukusanyaji wa kodi ya juu, kilionyesha sura yake ya umwagaji damu zaidi katika vipindi kama hiki.
 
Kipindi hiki cha utawala wa maeneo mengine, chenye dhamana za usalama na ukusanyaji wa kodi ya juu, kilionyesha sura yake ya umwagaji damu zaidi katika vipindi kama hiki.

"Jaribio lolote la uasi lilipigwa vita kwa kuonyesha wazi nguvu ya Roma, na kuwatisha waasi wa siku zijazo.
 
Vurugu ilikuwa alama ya amani hii ya Kirumi, amani ya makaburini, iliyopatikana kupitia vurugu, kwa kuwekewa utawala wa makazi," anasema Moraes.

"Yesu alionekana kuwa tatizo kubwa sana la kisiasa kwa mamlaka iliyoanzishwa. Roma ilijua kwamba Palestina ilikuwa ni kitovu cha upinzani na ilikuwa ni lazima kuushinda," anafupisha.
 
Chevitarese anasema kwamba ikiwa mazoezi ya kawaida yangekuwa hivi, kwa majaribio yaliyorekodiwa, baadhi ya habari juu ya maelfu ya kusulubiwa kulikofanyika zingesalia katika ungo wa wakati.

"Hebu tusahau kwa dakika moja kisa cha Yesu wa Nazareti na tufikirie juu ya maasi makubwa ya watumwa ambayo yalitikisa mwisho wa Jamhuri ya Kirumi.
 
Back
Top Bottom