Hizi ni ambazo nimezifanya ziwe kama mwongozo wako;
Afya
Afya ya Mwili. Afya ya Akili. Afya ya Kiroho. Vitu Hivi vitatu ni muhimu sana kwenye maisha yako. Huwezi kusema una maisha bora kama hizi sehemu tatu hazina ubora au hazina afya.Unapaswa kuwa na mikakati ya kufanyia kazi sehemu hizi kwasababu ndio zimebeba maisha yako yote
Hekima
Wakati Sahihi wa Kukaa Kimya. Wakati Sahihi wa Kuongea Kitu Sahihi Cha Kuongea. Hii itakuwezesha uweze kuishi na wengine vizuri. Kuna watu wenye tabia mbalimbali zinazokera bila ya Hekima utakuwa mtu mwenye hasira, chuki na Visasi hutaweza kufurahia maisha.
Utajiri
Uwekezaji, Mali, Mtandao wa Watu, Upendo.Maisha ili yawe bora ni lazima ufikie kile kiwango ambacho Hutakuwa na Matatizo yanayoletwa na ukosefu wa pesa.Hivyo ni muhimu kuhakikisha vile ambavyo unatakiwa kuvifanyia kazi ili kujenga mifereji ya kipato ambayo inadumu.
Kuna msemo unasema" kupanga ni kuchagua na kutenda ni kuamua" na hii ni siri kubwa iliyopo katika mafanikio yako. Unatakiwa kufanya tafakari makini juu ya kuchagua vitu muhimu vya kufanya katika maisha yako yote. Na kufanya uchaguzi wa mambo mbalimbali hakikisha ni mambo chanya.
Hivi hajawahi kutembelewa na ndugu, jamaa, au rafiki nyumbani kwako? Bila shaka umewahi, na je ulipomuuliza atatumia nini mgeni huyo kati ya juisi na maji , je alikujibu nini? Bila Shaka nafikiri alikwambia nitatumia chochote.
Majibu ya aina hii ndiyo ambayo yamesababisha maisha yetu kuwa magumu, wengi wetu tumekuwa hatujui ni nini ambacho tunachotaka, hali hiyo imepelekea kuwa tayari kufanya jambo lolote. Lakini ukweli ni kwamba maisha yako ili yawe bora ni lazima ujue ni kitu gani ambacho unataka.