Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

IMG_1049.jpg
 
Fanya mazoezi
Watu wengi hasa Waafrika hawana utaratibu wa kufanya mazoezi. Kufanya mazoezi kutakuwezesha viungo vyako vya mwili kufanya kazi ipasavyo. Ni dhahiri pia unapofanya mazoezi utatokwa na jasho; na hii ni njia nzuri ya kutoa taka mwilini ikiwemo sumu zilizoingia katika mwili wako. Unaweza kufanya mazoezi ndani au hata nje kutegemea vile unavyopendelea.
 
Punguza mafuta
Inawezekana unapenda kula vyakula vyenye mafuta mengi; hili si jambo zuri kwa ajili ya afya yako. Jizoeze kupunguza ama kuepuka mafuta katika vyakula vile unavyokula kwani si aina zote za mafuta zinafaa kwenye mwili wako
 
Hivi leo yapo mafuta yasiyo halisi yanayozalishwa viwandani, hivyo kula mafuta haya ni kuongeza sumu mwilini mwako. Pia ulishaji mbaya wa wanyama umepelekea mafuta ya wanyama kuwa na viambata vyenye sumu ambavyo havifai mwilini mwako – Kwa mfano nguruwe wanapewa ARV na Urea ili wakue haraka.
 
Vyakula vyenye nyuzinyuzi nyingi ni pamoja na parachichi, ndizi, peazi, karoti, pilipili hoho, mchele wa brown (wanaoutumia watu wa kisukari), maharage meusi, njegere, tende, viazi vitamu, tofaa (apple), machungwa, ugali wa dona pia mkate wa unga wa ngano ambao haujakobolewa. Ulaji wa vyakula hivi utakuwezesha kuondoa kiasi kikubwa cha sumu mwilini.
 
Kaa kwenye hewa safi na yakutosha
Nyumba za kuishi au mazingira mengi ya kazi Afrika bado hayajali sana afya za wakaazi wake. Ikumbukwe kuwa sumu nyingi zipo kwenye hewa kutokana na uchafuzi wa mazingira; hivyo mtu anapokaa mahali ambapo hakuna hewa safi ya kutosha, anaongeza hatari zaidi ya kuongeza sumu mwilini.
 
Back
Top Bottom