Ndizi hutuliza tumbo ikisaidiwa na asali, inayorejesha kiwango cha sukari kilichopungua kwenye damu wakati maziwa nayo hutuliza na kurejesha maji kwenye mfumo wake.
Pamoja na hayo ndizi pia husaidia katika matatizo mengi na kutuliza mishipa ya fahamu, kuondoa wasi wasi, kutuliza vidonda vya tumbo, tindikali na kushusha joto mwilini pamoja na kurekebisha mapigo ya moyo. n.k.
Asali ni tiba karibu kwa kila ugonjwa. Matumizi ya asali kama tiba kwa magonjwa mbalimbali ni kitu ambacho kinafahamika kwa karne nyingi zilizopita duniani kote. Vitabu vingi vya zamani vimeandika namna watu walivyotibiwa magonjwa mbalimbali kwa kutumia asali.
Dawa hii ya asili ni maarufu kwa maelfu ya miaka katika tiba asili za China (Traditional Chinese Medicine - TCM), Ugiriki (Unani Medicine), India (ayurvedic) na Mashariki ya kati (The science of medicines based on natural treatment in the East - Tibb).
Mdalasini pia una sifa ya kuondoa vivimbe, pia huondoa sumu mwilini. Vinapoungana vitu hivi viwili vya asili vinatengeneza muungano mmoja mhimu wa dawa dhidi ya maambukizi ya nje.
TIBA YA BARIDI YABISI (Arthritis)Watu wengi wanaripoti matokeo mazuri baada ya siku chache tu za kutumia kinywaji hiki chenye mchanganyiko wa asali yenye mdasini kutwa mara 2.
Ili kutibu baridi yabisi ongeza kijiko kidogo kimoja cha mdalasini ya unga na kijiko kikubwa kimoja cha asali mbichi ndani ya glasi 1 ya maji ya uvuguvugu na unywe nusu glasi kabla ya chakula cha asubuhi na nusu glasi nyingine kabla ya kwenda kulala.