Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

HUTIBU LEHEMU (Cholesterol)
Matumizi ya mara kwa mara ya asali yenye mdalasini husaidia kupunguza lehemu. Pia husaidia kushusha shinikizo la juu la damu na kusafisha ateri zinazoziba.
 
HUTIBU MAUMIVU YA JINO
Changanya kijiko kidogo kimoja cha chai cha mdalasini ya unga na vijiko vikubwa viwili vya asali mbichi na upake kidogo kidogo juu ya jino linalouma mara kadhaa kwa siku kila siku mpaka maumivu yatakapopotea.
 
HUONDOA HARUFU MBAYA MDOMONI
Changanya kijiko kikubwa kimoja cha asali na kiasi kingine sawa cha mdalasini ya unga ndani ya maji glasi moja ya uvuguvugu na unywe mara tu ukiamka asubuhi.
Hii itakutibu tatizo la harufu mbaya mdomoni na utapumua vizuri bila shida yoyote.
 
HUTIBU UANITHI NA KUKOSA HAMU YA TENDO LA NDOA

Jaribu na uone tofauti! Changanya vijiko vikubwa vitatu vya asali yenye mdalasini ndani ya glasi moja ya maji ya uvuguvugu na uache mchanganyiko huo kwa dakika 15 hivi.
 
HUONGEZA KINGA YA MWILI

Ongeza kinga yako ya mwili na magonjwa hayatakugusa. Vyote asali na mdalasini hupigana dhidi ya bakteria na virusi na hivyo kufanya dawa nzuri ya kupigana na kuua bakteria wabaya na virusi.
 
HUTIBU MAFUA

Tumia mchanganyiko wa kijiko 1 cha chakula cha asali yenye mdalasini ndani ya glasi moja ya maji ya uvuguvgugu kutwa mara moja kila siku kuondoa chafya na kuvimba koo.
 
HUTIBU UGUMBA

Asali inaaminika kuamsha hamu ya mapenzi. Wapenzi wa jinsia zote wanashauriwa kunywa walau vijiko viwili vya chakula kila siku kabla ya kwenda kulala kila siku.
 
FAIDA NYINGINE LUKUKI

Kumbuka asali ni dawa karibu kwa kila ugonjwa na watu wamekuwa wakiitumia kutibu magonjwa mengine mengi bila idadi ikiwemo matatizo ya kisukari, kukakamaa kwa miguu na mikono, udhaifu wa jumla wa mwili, kuongeza kumbukumbu, vidonda vya tumbo, kutibu majeraha nk nk
 
NAMNA YA KUANDAA NA KUITUMIA ASALI YENYE MDALASINI
Kwenye lita 1 ya asali ongeza vijiko vikubwa vitano vya mdalasini ya unga na ukoroge vizuri kabla ya kuutumia. Uhifadhi mchanganyiko huu kwenye bakuli kubwa ili iwe rahisi kuukoroga tena vizuri kila unapotaka kuutumia.
 
Ceylon cinnamon
Mdalasini ambao hutumika kama dawa hujulikana kwa kitaalamu kama ‘Ceylon cinnamon’ na kwa kawaida wenyewe huuzwa gharama sana
 
Back
Top Bottom