Newcastle wanajiandaa kumsajili mlinda mlango wa PSG Keylor Navas, ambaye atawahama vinara hao wa Ligue 1, lakini mkongwe huyo wa Costa Rica, mwenye miaka 35 anasakwa pia na Juventus na Sevilla. (Fichajes - in Spanish)
Licha ya West ham kusisitiza kwamba kiungo huyo wa England hauzwi inaelezwa kwamba wanaweza kukubali ofa ya £150m kwa ajili ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 23, anayesakwa pia na vilabu vya Manchester United na Chelsea. (The Guardian)
Celtic wako katika mazungumzo ya mwisho na Tottenham kwa ajili ya kumsajili mlinzi wa kati wa Marekani Cameron Carter-Vickers, 24, kwa uhamisho wa kudumu. (SBI Soccer)
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 29 atakua huru mwishoni mwa msimu lakini atazingatia kuhamia klabu zitakazocheza ligi ya mabingwa Ulaya msimu ujao. (Ben Jacobs, CBS)
Wayne Rooney amekataa ofa ya kufanya kazi kama msaidizi wa Erik ten Hag pale Manchester United, akisisitiza kwamba ataondoka tu Derby County akipata ofa ya kuwa meneja na sio msaidizi. (Athletic, subscription required)
Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, West Ham na Manchester City Carlos Tevez anaweza kurejea kucheza soka karibu mwaka mmoja baada ya nyota huyo mwenye miaka 38 kucheza mchezo wake wa mwisho akiwa na Boca Juniors.