Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hawasomi tu vitabu au makala, bali wanasoma vile ambavyo vina ubora na maarifa stahiki. Kwa njia hii wanafahamu mambo mengi na kuwafanya kutoa hoja zenye ushahidi na ufafanuzi wa uhakika.
 
Wanachangamana na watu


“Kwenye watu kuna mengi.”

Watu wanaofahamu mambo mengi wanapenda kuchangamana na watu pamoja na kujenga mtandao wa mahusiano. Watu hawa huhakikisha wanajenga mahusiano na watu sahihi hasa wale wanaofahamu mambo mengi
 
Wanatazama na kusikiliza vitu vingi vya kuelimisha

Watu wanaofahamu mambo mengi wanatazama na kusikiliza vitu vyenye kuelimisha. Ni rahisi kumkuta mtu wa kawaida akitazama mziki au maigizo siku nzima; lakini watu wanaofahamu mambo mengi hawafanyi hivyo.
 
Wana shauku ya kujifunza

Huwezi kufahamu mambo mengi kama huna shauku ya kujifunza. Watu wanaofahamu mambo mengi hutamani kila mara kujifunza jambo jipya.

Hili huwafanya watafute maarifa na kutafiti juu ya mambo mbalimbali kila mara kwenye maisha yao.
 
Wanafundisha watu wengine


“Mwalimu ni mwanafunzi wa kudumu.”

Huwezi kuwafundisha watu wengine jambo ambalo wewe hulifahamu. Kwa njia ya kuwafundisha watu wengine, watu wanaofahamu mambo mengi hujifunza mambo mbalimbali kila siku ili waweze kupata maarifa ya kuwafundisha wengine.
 
Hushughulikia maendeleo yao binafsi


Ni watu wachache sana ndio wanafahamu umuhimu wa kuboresha au kujali swala la maendeleo yao binafsi. Watu wanaofahamu mambo mengi kila siku hutafiti na kutafuta mbinu na njia za kuwafanya kuwa bora zaidi
 
Watu wanaofahamu mambo mengi hujishughulisha mambo kama vile kuongeza uwezo wao wa lugha, matumizi sahihi ya muda, kuboresha afya, kuongeza kipato, kuongeza ufanisi wa utendaji wao wakazi, n.k.

Kwa njia hii wanapata maarifa zaidi yanayowafanya kufahamu mengi na kuwa tofauti na wengine.
 
Hawaridhiki kirahisi


Kuridhika ni muhimu sana maishani, lakini kuridhika bila kitu hakuna maana yoyote. Watu wanaofahamu mambo mengi hawaridhiki kirahisi na yale wanayoyafahamu au vile walivyonavyo.

Watu hawa kila mara hutafiti na kuchunguza mambo mbalimbali ili kuongeza kiwango chao cha maarifa.
 
Wanasafiri sana

“Kutembea ni kuona mengi.”

Naamini umewahi kusikia kauli mbalimbali kamavile tembea uone mengi, mkaa bure si sawa na mtembea bure, n.k. Pasipo shaka, kauli hizi zinadhihirisha ukweli kuwa kutembea au kusafiri kuna manufaa mengi.
 
Back
Top Bottom