Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Haya hayapo tu katika nchi za Ulaya kama vile Uingereza, Ufaransa na Norway, lakini pia Polinesia ya Ufaransa na Maldives, ambapo kupanda kwa kina cha bahari katika taifa hilo la Bahari ya Hindi sasa kunaleta tishio kubwa.
 
Tofauti na boti za nyumba, ambazo zinaweza kufunguliwa kwa urahisi na kuhamishwa, nyumba zinazoelea zimewekwa kwenye ufuo, mara nyingi zikifungiwa kwa chuma, na kwa kawaida huunganishwa na mfumo mkuu wa maji taka na umeme.
 
Kwa miji inayokabiliwa na mafuriko yanayozidi kuwa mbaya na uhaba wa ardhi kwa ajili ya makazi, nyumba zinazoelea ni mojawapo ya mwongozo wa kupanua makazi ya mijini katika enzi ya mabadiliko ya hali ya hewa.
 
Koen Olthuis, ambaye mwaka 2003 alianzisha Waterstudio, kampuni ya usanifu ya Uholanzi inayohusika na kujenga majengo yanayoelea, anasema teknolojia ya chini ya nyumba zinazoelea ni uwezekano wa faida yao kubwa.
 
Nyumba anazobuni zimeimarishwa na nguzo zilizochimbwa takriban mita 65 (futi 210) ardhini na kuwekewa nyenzo ili kupunguza hisia za kusonga kutoka kwa mawimbi. Nyumba hupanda maji yanapopanda na kushuka wakati maji yanapungua.
 
anasema Marjan de Blok, mkurugenzi wa TV ya Uholanzi ambaye alianzisha mradi huo mwaka wa 2009 kwa kuwakusanya wasanifu wamajengo, wataalam wa sheria, wahandisi na wakazi ambao walifanya kazi ili kuuanzisha mradi huo.
 
Back
Top Bottom